Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla amemsimamisha kazi Meneja wa Pori la Akiba Uwanda, katika wailaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Mark Chuwa kwa tuhuma za kushindwa kuondoa mifugo zaidi ya 12,000 iliyopo ndani ya hifadhi hiyo.
Kabla ya uamuzi huo, akisoma taarifa ya mkoa kwa Waziri huyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk. Khalfan Haule alisema uvamizi katika pori hilo umekuwa wa kiasi kikubwa ambapo wafugaji huingia na makundi makubwa ya mifugo na kugeuza eneo hilo sehemu ya malisho.
Alisema licha ya na kufanyika kwa opresheni za mara kwa mara za kuondoa mifugo hiyo, baada ya muda mfupi wafugaji hao hurejea na makundi makubwa ya mifugo kwa ajili ya malisho.
Hata hivyo Dk. Kigwangalla alishangazwa na uongozi wa mkoa na wilaya kwa kushindwa kuchukua hatua za kuondoa mifugo hiyo hifadhini wakati sheria za uhifadhi haziruhusu mifugo hifadhini.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa