• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA USAFIRISHWAJI WA MBOLEA

imewekwa Tar: January 10th, 2018

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na usafirishaji wa mbolea kutoka wa wasambazaji wa pembejeo nchini kwenda kwa wakulima. 

Pia ameitaka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuwa na mikakati madhubuti itakayowezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati wote nchini. 

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Januari 10, 2018) wakati akikagua usafirishaji wa mbolea kwenye maghala makubwa matatu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji kuona wakulima wote nchini wanapata pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea kwa wakati ili kilimo kiweze kuwaletea tija.

Amesema TFC inatakiwa ianze maandalizi ya usambazaji wa mbolea mapema kwani Serikali inataka wakulima wapate pembejeo miezi miwili kabla ya kuanza kwa msimu. 

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akutane na wadau na kufanya mapitio ya gharama za usafirishaji wa mbolea.

Amesema lengo la mapitio hayo ni kuhakikisha mkulima aliyeko kijijini anapata  mbolea hiyo kwa gharama nafuu bila ya kumuathiri mfanyabiashara.

Pia amemtakaDkt. Tezeba ashirikiane na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba ili kuhakikisha malori yanayobeba mbolea yanafika katika mikoa husika kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Kilimo awasiliane na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbawala ili malori yanayobeba mbolea yakifika kwenye vituo vya mizani yapewe kipaumbele.

 

“Si kwamba yaongeze uzito hapana, bali yapewe kipaumbele cha kupima haraka ili yaweze kuwahisha mbolea kwa wakulima kwani tayari msimu umeshaanza.”

Naye Waziri wa Kilimo, Dkt. Tizeba alisema watahakikisha mbolea ya kutosha inakuwepo nchini na kwamba wakulima wote wanaipata kwa wakati na kwa gharama nafuu.

 

Maghala aliyoyakagua Waziri Mkuu ni ghala la Mohammed Enterprises lililoko Mbagala, ghala la  Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) lililoko Kurasini na ghala la Premium lililoko Vingunguti ambako kote amekuta malori yakipakia mbolea kwa ajili ya uisafirisha katika mikoa mbalimbali nchini.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MADAKTARI BINGWA 33 WAPOKELEWA RUKWA, HUDUMA ZA KIBINGWA KUTOLEWA HOSPITALI ZA WILAYA KWA SIKU TANO

    May 19, 2025
  • RUKWA YAANZA RASMI MATUMIZI YA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI KWA ZAO LA MBAAZI NA UFUTA

    May 13, 2025
  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa