• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda awataka watumishi Rukwa kupambana na udumavu.

imewekwa Tar: November 20th, 2019

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mizengo Pinda amewasisitiza watumishi mkoani Rukwa kuhakikisha kila mmoja katika nafasi yake anafanya kazi kwa uadilifu na kueleza kuwa utendaji kazi wa aina hiyo ndio njia pekee ya kupeleka maendeleo ya mkoa mbele na hatimae kuutoa mkoa katika umasikini.

Amesema kuwa amesikitishwa na taarifa iliyolewa hivi karibuni kuhusu hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2018 ambapo mkoa wa rukwa umeonekana kushika mkia kwa kuwa na asilimia 45 ya umasikini nchini kwa mahitaji ya msingi huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa na asilimia 8 ya kiwango hicho huku mkoa wa Katavi uliozaliwa kutoka mkoa wa rukwa ukiwa na asilimia 29

Pia ameshtushwa kuwa mkoa wa Rukwa ambao ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa uzalishaji wa chakula nchini kuwa na kiwango kikubwa cha udumavu pamoja na kuongoza kuwa na kiwango kikubwa cha umasikini wa chakula kwa asilimia 19 wakati Katavi ukiwa na asilimia 9.

“Tukikaa sisi kama wataalamu, najua baadhi ya wilaya wameshapata maafisa lishe, tutawatengenezea mfumo tuwaonganishe na majukumu ya zahanati na vituo vya afya na hospitali zetu za wilaya, mama anapokuwa ametunga mimba lazima aambiwe aende kliniki, lakini kliniki si kupima tu uzito nakadhalika, hapana, kubwa ni kuona kwamba huyu mama mzazi anapata lishe stahiki?” Alihoji.

Amesema kuwa fikra zilizopo katika makabila yaliyopo mkoa wa Rukwa na Katavi wanaamini kuwa kula mboga za majani ni umasikini wa kutupwa kwahiyo kama mkoa una kazi kubwa ya kubadili fikra za watu hao na kuonyesha umuhimu wa kula mboga za majani.

Ameyasema hayo katika salamu zake kwa watumishi wa mkoa wa Rukwa hivi karibuni ambapo kikao hicho kiliwajumuisha wakuu wa taasisi, idara, wakala za serikali pamoja na watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mh. Joachim Wangabo.

Wakati akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Joachim Wangabo alimpongeza Mh. Pinda kwa kuhakikisha anasogeza huduma muhimu kwa wananchi kwa kuugawa mkoa wa Rukwa na kuzaliwa Mkoa wa Katavi ambapo hivi sasa wananchi wa mkoa wa Katavi wanafaidika na maendeleo yanayopatikana kutokana na uwepo wa huduma muhimu za kijamii katika halmashauri tano za mkoa huo.

“ Wilaya ya Mpanda ilikuwa inapakana na Kaliua, Uvinza na inapakana na Sikonge Mkoa wa Tabora, Sasa fikiria huyo RC aliyekuwa anatoka Sumbawanga kwenda mpaka huko, huenda ukakaa miaka mitano usifike maeneo mingine, ilikuwa ni shida kweli na miundombinu yake ilikuwa ni matatizo makubwa sana kwahiyo kuugawa huu mkoa wa Rukwa kuwa mikoa miwili umetoa unafuu mkubwa sana wa kimaendeleo” Alisema.

Mkoa wa Rukwa ulianzishwa mwaka 1974 kwa kumega sehemu ya Mikoa ya Tabora na Mbeya. Mkoa una eneo la kilomita za mraba 27,765,  kati ya hizo Kilomita za mraba 22,844 (82.3%) ni za nchi kavu na Kilomita za mraba 4,921 (17.7%) ni za maji. Mkoa una jumla ya Wilaya tatu (3), zenye Halmashauri nne (4), Tarafa 16, Kata 97, Vijiji 339, Vitongoji 1,825, Mitaa 167 na Kaya 199,766. Mwaka 2010 mkoa uligawanywa na kuzaliwa mkoa wa Katavi.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MADAKTARI BINGWA 33 WAPOKELEWA RUKWA, HUDUMA ZA KIBINGWA KUTOLEWA HOSPITALI ZA WILAYA KWA SIKU TANO

    May 19, 2025
  • RUKWA YAANZA RASMI MATUMIZI YA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI KWA ZAO LA MBAAZI NA UFUTA

    May 13, 2025
  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa