• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kupelekea kuanzishwa kwa shule mpya.

imewekwa Tar: January 6th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameishauri Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuona namna ya kuanzisha shule mpya ili kuleta uwiano wa waalimu katika shule hizo unaoendana na idadi ya wanafunzi ambao wanatarajiwa kuongezeka kila mwaka mpya wa masomo.

Ameyasema hayo aliposhiriki kwenye songambele ya ujenzi wa madarasa nane ya Shule ya Sekondari Kirando yanayotarajiwa kutumiwa na wanafunzi 422 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 katika shule hiyo inayobeba wanafunzi kutoka katika kata mbili zilizopo wilayani Nkasi.

“tunapoangalia kutatua changamoto ya shule hii ya Kirando Sekondari tuangalie ufumbuzi wa kudumu zaidi, muangalie uwezekano wa kujenga shule nyingine, huo ndio utakuwa ufumbuzi, shule hii ina O – level na A – level, sasa kama kutakuwa na shule nyingine ya O – level peke yake na hii mkaipunguzia mzigo wa kuchukua wanafunzi wengi na walimu wengi katika shule moja”

Ametoa rai kuwa kwa eneo la ekari 60 linalomilikiwa na shule hiyo ya Sekondari Kirando inawezekana kugawa walau ekari 20 kwa shule hiyo mpya jambo litakalowapelekea kupewa waalimu wapya kwa shule mpya na kuleta uwiano wa waalimu kuliko hali ilivyo sasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda aliyapokea maagizo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kuanzia ngazi ya Kijiji hadi ngazi ya halmashauri ya Wilaya na kuongeza kuwa suala hilo litawekwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019 na kuongeza kuwa wananfunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza watasioma.

“wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza katika shule hii ya Kirando ni 422 na tumekubaliana kuwa hadi kufungua shule wananfunzi wote hao wanatakiwa wawe madarasani, lakini tumekubaliana na wazazi kuwa kama serikali tutanunua meza zote 422, lakini tumewahamasisha kuchangia walau mchango wa kiti ili mwanafunzi anapokuja akute meza na kiti ili tulimalize jambo hilo,”

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari kirando Erneo Mgina akitoa taarifa fupi ya shule hiyo alisema kuwa shule ina wanafunzi 677 na kutaraji kupokea wanafunzi 422 na upungufu wa madara nane ambayo matatu tayari na mengine yapo katika hatua ya msingi na kutaraji kurekebisha vyumba vitatu vya maabara ili kuwahifadhi wanafunzi kwa muda hadi madarasa yatakapokamilika.

Hili limekuja ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI kuitaka mikoa iliyokuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 ukiwemo mkoa wa Rukwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata madarasa ya kusomea, madawati na vyoo pale shule zitakapofunguliwa tarehe 8/1/2018.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa