Wizara ya Afya kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la Pathfinder imetoa mafunzo elekezi kwa waratibu wa huduma ya M-Mama Mkoani Rukwa.
Mafunzo hayo yaliyowahusisha waratibu wa huduma hiyo kwa ngazi ya Mkoa na Halmashauri yametolewa katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Julai 8, 2024.
Akizungumza na waratibu hao Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Bw. Martin Mbogo amewataka waratibu kuimarisha matumizi ya huduma ya M-Mama na kuwaasa kuendelea kusimamia taaluma na kujitoa ili kuendelea kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na watoto.
Kwa upande wake mratibu wa Huduma ya Mama na Mtoto Mkoa wa Rukwa Bi. Asha Ressa Izina ameeleza kuwa pamoja na mafunzo hayo imefanyika tathmini ya utekelezaji wa huduma hiyo Mkoani Rukwa kwa Mwaka 2023/24 na kubaini kuwa zipo Halmashauri ambazo zimekuwa na matumizi madogo sana ya fedha kwenye mfumo na nyingine zikiwa hazijatumia kabisa.
M-mama ni huduma ya usafiri wa dharura nafuu inayowaunganisha akina mama na watoto wachanga kwenye huduma muhimu ya kuokoa maisha katika maeneo ya vijijini Tanzania.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa