Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika Mkoa wetu ikiwemo ujenzi wa daraja kubwa lenye urefu wa mita 84 linajengwa eneo la Kilyamatundu/ Kamsamba katika Mto Momba kwa gharama ya Shilingi 17.7 Bilioni. Ujenzi wa Daraja hili ulianza tarehe 1 Agosti, 2017 na lilipaswa kukamilika baada ya miezi 13 yani 31 Agosti, 2018. Aidha, kutokana na changamoto ya mafuriko ya Mto Momba wakati wa mvua za masika kazi za ujenzi ziliahirishwa hivyo, ujenzi huo sasa utakamilika Mwezi Februari, 2019. Hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 65 ambapo tayari mkandarasi amekwishajenga nguzo (pivers) mbili na kingo (abutments) mbili za upande wa Kilyamatundu na Kamsamba pia ujenzi wa beams na sakafu (deck slab) umekamilika. Kukamilika kwa Daraja hili kutaongeza fursa za kiuchumi katika eneo la Bonde la Ziwa Rukwa hivyo kuendelea kuifungua Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa