Programu ya Maendeleleo ya Kilimo (ASDP I)
Mkoa wa Rukwa umekuwa ukitekeleza programu ya maendeleleo ya Kilimo ASDP tangu mwaka 2007. Programu ya Maendeleo ya Kilimo (ASDP I) muda wake wa kutekeleza uliisha mwaka 2013/2014. Shuguli muhimu zilizotekelezwa na Programu hii zilikuwa ni:-
Kuwawezesha wakulima kuongeza tija katika mazao ya kilimo na Mifugo
Kujenga miundombinu ya masoko
Kujenga miundombinu ya skimu za umwagiliaji
Kuwajengea uwezo wataalam wa kilimo katika ngazi za Halmashauri na Mkoa
Kukarabati na kujenga majosho
Kujenga miundombinu ya maji kwa ajili ya mifugo
Kwa Miaka miwili ya 2014/2015 na 2015/16 Programu hii ipo katika kipindi cha mpito kuelekea awamu ya pili. Mpaka kufikia Desemba 2015 Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kupitia Wizara ya OR - TAMISEMI walituma Rasmu ya ASDP II kwa ajili ya kutoa maoni na Mkoa ulishawasilisha maoni ya Rasmu hiyo.
Vituo vya Rasilimali za Kilimo (WARCs)
Mkoa wa Rukwa una jumla ya Vituo vya rasilimali za Kilimo 9 (Kalambo DC 1, Nkasi DC 5, Sumbawanga DC 2 na Sumbawanga MC 1). Vituo hivyo vinatumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakulima, kupata machapisho rejea, kupata teknolojia za Kilimo kwa wakulima waliopo katika Kata.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa