Hadi sasa Serikali imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 4.1 zilizotumika kujenga na kukarabati vituo vya Afya vifuatavyo:-
Kituo cha Afya Mazwi - Shilingi 500,000,000/=
Kituo cha Afya Katumba Azimio - Shilingi 400,000,000/=
Kituo cha Afya Nkomolo - Shilingi 500,000,000/=
Kituo cha Afya Kirando - Shilingi 400,000,000/=
Kituo cha Afya Wampembe- Shilingi 400,000,000/=
Kituo cha Afya Milepa - Shilingi 400,000,000/=
Kituo cha Afya Legezamwendo - Shilingi 700,000,000/=
Kituo cha Afya Mwimbi - Shilingi 400,000,000/=
Kituo cha Afya Kanyezi - Shilingi 400,000,000/=
Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kila Wilaya inakuwa na Hospitali ya Wilaya. Kwa Mkoa wetu zitajengwa Hospitali tatu kwa maana Halmashauri ya Sumbawanga Vijiji (Mtowisa), Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (Eneo la Mkangale- Namanyere) na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo eneo la Matai. Hospitali zote hizi zimetengewa kiasi cha Shilingi 1.5 bilioni kila moja na tayari kila Halmashauri imeshapokea kiasi cha Shilingi 500,000,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Aidha, ili kuendelea kuboresha huduma za afya katika ngazi za Vijiji Mkoa umefanikiwa kuongeza Zahanati kutoka 181 mwaka 2015 hadi 200 mwaka 2018. Hata hivyo ujenzi wa maboma ya Zahanati 60 unaendelea katika Mkoa wetu.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa