Moja ya kibanda cha kilichokuwa katika kambi ya Wavuvi ya Mererani kikiwaka moto ikiwa ni juhudi za kuwaondoa wavuvi waliopo ndani ya Ziwa Rukwa kuwaepusha na kipindupindu na kulinda ziwa lisipotee.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa kwanza mbele kulia) akiwa ameambatana na mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule walipotembelea kambi ya mererani waliyohamishwa wavuvi kwa nguvu ili kuepuka kipindupindu na kulinda mazingira ya ziwa hilo.
Miongoni mwa wananchi waliokuwa wakiishi katika makambi ya wavuvi yalipo ndani ya Ziwa Rukwa yaliyoathiriwa na kipindupindu wakisimamiwa kuhama kambi hiyo ili kujiepusha na kipindupindu na kuliza Ziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa tahadhari kwa Wavuvi waliohamishwa kwenye makambi (hawapo pichani) kutorudi katika makambi hayo kwa usalama wa afya zao na kuendelea kulitunza ziwa Rukwa.
Miongoni mwa Vyoo vinavyotumiwa na Wavuvi wa kambi ya Nankanga waliopewa miezi mitatu kuihama kambi hiyo kabla ya kipindupindu kuwamaliza.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipoongozana na kamati ya ulinzi na Usalama kuangalia moja ya choo kinachotumiwa na wavuvi wa kambi ya Nankanga, choo ambacho si salama kwa matumizi ya binadamu.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule akichoma nyavu haramu moto walizozipata katika kambi ya Mererani Kijiji cha Ilanga walipowahamisha watu kwaajili ya kuepuka kipindupindu kwa kutokuwa na vyoo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa ACP George S. Kyando akiendelea kuchoma nyavu haramu moto walizozipata katika kambi ya Mererani Kijiji cha Ilanga walipowahamisha watu kwaajili ya kuepuka kipindupindu kwa kutokuwa na vyoo.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa