MIPANGO YA MAENDELEO YA MKOA 2016/2017 - 2020/2021
Vipaumbele vya Mkoa wa Rukwa
a) Uboreshaji wa Miundombinu ya mawasiliano ya Barabara, Bandari, Reli, TEHAMA, na usafiri wa anga
b) kusimamia Mapinduzi ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kisayansi zaidi ili kuleta tija na mageuzimakubwa ya kiuchumi Mkoani Rukwa;
c) Uboreshaji wa huduma za jamii (Elimu, Maji, Afya & UKIMWI) Maendeleo ya Watumishi, Hifadhi ya Mazingira;
d) Kujenga mzingira mazuri ya Biashara na Uwekezaji wa Viwanda vidogo, vya kati na vikubwa;
e) Uendeshaji wa Ardhi na Makazi katika maeneo yote ya Mkoa wa Rukwa.
f) Kuimarisha Ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Mpango wa Maendeleo wa miaka Mitano kwa mwaka 2016/2017 - 2020/2021 imeandaliwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo;
a) Mpango wa Mkoa wa Rukwa wa maendeleo wa miaka 10 wa 2010/2011 - 2020/2021
b) Mpango wa pili wa maendeleo ya miaka 5 2016/2017 - 2020/2021
c) Mwongozo wa maandalizi ya bajeti ulioandaliwa na kutolewa na Wizara ya Fedha na Mipango mwezi January 2016;
d) Sheria ya bajeti Namba 11 ya mwaka 2015 na Kanuni zake za mwaka 2015,
e) Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025;
f) Mkakati wa Kukuza na Kupunguza Umaskini - MKUKUTA;
g) Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015
h) Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (United Nations Sustauinable Development Goals - SDGs);
i) Sera mbalimbali za Taifa na Kisekta, na kauli mbiu za Kilimo Kwanza, Mfumo wa Tekeleza sasa kwa Matokeo Makubwa (Big Result Now) na uwekaji wa mazingira mazuri ya uendeshaji wa Viwanda;
j) Pamoja na vipaumbele vya Mkoa wa Rukwa ambavyo ni uboreshaji wa Miundombinu, Kilimo, Huduma za Jamii (Elimu, Maji, Afya & UKIMWI) Maendeleo ya Watumishi, Mazingira, kujenga mazingira mazuri ya Uwekezaji wa Viwanda,
pamoja na Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa