SEKTA YA UTALII.
Mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii umeendelea kutambua maeneo yenye fursa za kitalii na kuyaboresha ili yaweze kuvutia watalii wengi katika Mkoa wetu. Mkoa wa Rukwa unavivutio vya watalii vifuatavyo:-
Maporomoko ya Mto Kalambo(Kalambo Falls)
Katika msitu wa Hifadhi wa Moporomoko ya Kalambo, Yapo Maporomoko makubwa ambayo ndio yanaleta jina la msitu huo na ni maarufu sana duniani.
Katika kipindi cha mwaka 2017/2018 tumeendelea kuboresha kivutio cha maporomoko ya mto Kalambo kwa kufanya maboresho yafutayo:
Kuimarisha Mpaka wa Hifadhi kwa kufyeka Kilomita 30 za mpaka na kuweka vigingi 83 kuzunguka hifadhi.
Kuratibu uanzishwaji na kuendeleza utalii Ikolojia katika eneo la maporomoko ya Kalambo.
Kutangaza maporomoko ya Kalambo katika mitandao ya Kijamii na kuongeza umaarufu wa hifadhi.
Kuandaa mchoro wa kujenga kituo cha Utalii ambacho kinajumuisha geti, Ofisi ya Meneja, Kituo cha habari kwa Watalii, Ukumbi, Kituo cha Utamaduni pamoja na Huduma za Jamii na maeneo ya uwekezaji.
Kupanga eneo la kujenga vyumba vya kulala Wageni, maduka, migahawa na zahanati
Kuweka mabango ya kutambulisha maporomoko (katika Kijiji cha Kapozwa)
Kujenga ngazi za kuteremka kwenye maporomoko zenye urefu wa mita 227 kwenye ukingo wa korongo la Mto Kalambo ambapo kazi hii inaendelea.
Maporomoko ya Kalambo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
Ngazi zitakazokupeleka maji yanapodondokea.
Ngazi zitakazokupeleka maji yanapodondokea.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa