Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuanzisha mchakato wa kinidhamu na uchunguzi mara moja dhidi ya Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wialaya ya Kalambo kutokana na utendaji kazi wake usioriddhisha.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amefafanua sababu kadhaa zilizosababisha Mkoa wa Rukwa kuongoza kwa utoro katika hotuba ya Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa alipokuwa akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Geita mapema mwezi huu.
Pia ameeleza mikakati kadhaa ya kukabiliana na utoro huo ikiwemo kusimamia programu ya chakula kwa wanafunzi ili kuwawezesha kuwa na moyo wa kusoma wawapo mashuleni.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amefanikisha kupatikana kwa ekari 3 ili kujengwa kwa nyumba za askari polisi katika eneo la karibu na kituo cha polisi kipya kinachomaliziwa kujengwa katika kata ya Mtowisa, Wilayani Sumbawanga na kurahisisha makazi ya polisi katika bonde la ziwa Rukwa.
Hayo yamejiri ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya wananchi wa kata ya Mtowisa kwa Mkuu wa Mkoa waliyoiahidi tarehe 13.11.2017 Mh. Wanagabo alipofanya ziara katika eneo hilo na kudai kuwa usalama wa bonde hilo sio mzuri kwa kukosa kituo bora cha polisi na makazi yao na kupelekea kuanzisha ujenzi wa kituo na hatimae kuomba nguvu ya Mkuu wa Mkoa kuweza kumalizia ujenzi huo.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa