Kaimu Meneja wa Wakala wa Misitu Wilaya ya Kalambo aelezea maajabu yanayopatikana katika maporomoko ya Kalambo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amepiga marufuku mwalo wa mwambao wa Kijiji cha Kirando kutumika kama bandari baada ya kufika katika mwalo huo na kukuta lori likiwa linapakua mizigo kwa lengo la kusafisirisha mizigo kwenda kwenye visiwa vya ziwa Tanganyika. Amesema kuwa wananchi wasipotoshe malengo ya mwalo huo ambayo ni kwaajili ya kuuza na kununua samaki wavuliwao kwenye ziwa Tanganyika, “Lengo la Mwalo huu ni kuuzia samaki na dagaa lakini naona mizigo hii, imegeuzwa kuwa bandari, narudia aliyoyasema Mh. Mbunge (Ali Kessy) irudishwe kwenye hali yake ile ile,” Alisisitiza
Uongozi wa Waislamu Mkoani Rukwa umepokea kwa furaha mchango wa Shilingi Milioni 5.7 uliotolewa na uongozi wa serikali ya Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika kikao cha maridhiano juu ya ujenzi wa msikiti uliosimama kwa muda. Fedha hizo zilizochangwa zilijumuisha ahadi, fedha taslimu pamoja na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa kwa umoja wa viongozi wa serikali kuonesha mshikamano uliopo kati ya serikali na wananchi bilaya kujali itikadi, dini wala rangi huku Mh. Wangabo akichangia milioni 1.5
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa