Mkuu wa Mkoa wa rukwa Mh. Joachim Wangabo ameeleza tukio la vifo vya watoto wawili kwa masikitoko makubwa, tukio lililohusishwa na imani za kishirikina katika Mkoa huo na kutoa pole kwa wafiwa wa mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite Sumbawanga Mjini.
Katika kuelekea siku ya upandaji miti kimkoa ambayo hufanyika kila tarehe 19 ya mwezi wa kwanza kila mwaka Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaasa wananchi pamoja na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kufika katika ofisi za wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ili kuweza kupatiwa miche ya miti na kuweza kuipanda katika maeneo yao.
Amesema kuwa TFS wametenga miche 100,000 kwaajili ya kutoa bure kwa taasisi pamoja na wananchi ambao watachangia kiasi cha shilingi 150 kwa mti mmoja na kuongeza kuwa kuchukua miti hiyo na kuipanda kutaiwezesha taasisi ama mwananchi kuwekeza katika miti, kupendezesha eneo lake hali itakayopelekea kupendezesha mandhari ya mkoa kwa ujumla.
Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule ambaye pia alikuwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alikwenda kuzitembelea kaya 336 zilizoathiriwa na mvua na upepo mkali uliotokea usiku wa tarehe 8.12.2018 na kuahidi kutoa kilo 5 za unga wa sembe kwa kila kaya kama kianzio huku misaaada mingine ikiendelea kusubiriwa
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa