Hali ya huduma ya maji katika Mkoa wa Rukwa kwa mwaka 2023/2024
Hadi kufikia mwezi June , 2023 asilimia 56.3 ya wakazi wa Mkoa wetu wanapata huduma ya maji safi na salama. Maji haya yanapatikana kutokana na programu mbali mbali ikiwemo NORAD, RUDEP, TASAF, Quickwins na WSDP (Water Sector Development Programu). Programu ya WSDP ndiyo ambayo inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji kwa sasa.
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini katika kila Wilaya
Na |
Halmashauri |
Idadi ya Watu |
Idadi ya Watu wanaopata huduma ya maji. |
Idadi ya Vituo vya Kuchotea Maji/Wateja |
Asilimia ya upatikanaji wa huduma ya Maji |
1 |
Sumbawanga MC (Mjini)
|
136,414 |
106,400 |
8,871 |
78 |
2 |
Sumbawanga MC (Vijijini)
|
121,016 |
87,132 |
307 |
72 |
3 |
Sumbawanga DC
|
494,330 |
237,278 |
717 |
48 |
4 |
Nkasi DC
|
425,420 |
216,964 |
934 |
51 |
5 |
Namanyere
|
38,143 |
7,630 |
246 |
20 |
6 |
Kalambo DC
|
316,783 |
161,243 |
526 |
50 |
JUMLA
|
1,134,693 |
634,502 |
11,601 |
56.3 |
Katika kuhakikisha huduma ya maji inaongezeka, Katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 Wizara ya Maji ilitenga kiasi cha shilingi 10,616,484,240 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa miradi ya maji na kampeni ya usafi wa mazingira.
Aidha Hadi kufikia Juni 2023, RUWASA Mkoa wa Rukwa walikuwa wameepokea kiasi cha Shilingi 15,521,029,437.20 kwa ajili ya Utekelezeaji wa Miradi ya Maji na Matumizi ya Kawaida
Mpango wa Kuongeza Upatikanaji wa Huduma ya Maji Vijijini
Mkoa una jumla ya miradi 10 yenye thamani ya shilingi 22,152,959,582.86 ambayo inatekelezwa katika Wilaya za Nkasi miradi 6, Kalambo miradi 2 na Sumbawanga miradi 2 kupitia Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira. Ili kuhakikisha miradi ya maji inakuwa endelevu, uundwaji na usajili wa vyombo vya watumia maji umefanyika katika baadhi ya miradi iliyokamilika na uundwaji unaendelea katika baadhi ya miradi iliyokamilika na inayoendelea na ujenzi. Hadi Juni , 2023 Mkoa una jumla ya vyombo vya watumia maji (COWSOs) 41, vinavyohudumia vijiji 325, ambavyo vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria Na. 12 ya mwaka 2009.
Wilaya ya Sumbawanga ina vyombo vya watumia maji (CBWSOs) 11 vinavyohudumia vijiji 138, Wilaya ya Kalambo ina vyombo vya watumia maji (CBWSOs) 18 vinavyohudumia vijiji 97 na Wilaya ya Nkasi ina vyombo vya watumia maji (CBWSOs) 12 vinavyohudumia vijiji 90
Mpango wa Kuongeza Upatikanaji wa Huduma ya Maji Mijini
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kupitia Mamlaka ya maji (SUWASA) imetekeleza mradi wa maji ujulikanao kama Mradi wa muda wa kati wa kusambaza maji na usafi wa mazingira. Mradi umetekelezwa kwa fedha za EU na Serikali ya Ujerumani kupitia KfW ambapo umegharimu Euro 14,593,444.68. Ujenzi wa mradi ulianza tarehe 18/03/2013 na umekamilika mwezi Desemba, 2017 na unatoa huduma kwa wananchi. Baada ya mradi kukamilika na kuanza kutumika imepelekea maeneo ya kutoa huduma (Service coverage) kwenye eneo lenye mtandao kuongezeka kutoka asilimia 51% kabla ya mradi hadi 78% kwa sasa
Mji Mdogo wa Namanyere
Katika Mji wa Namanyere mradi uliotekelezwa ni wa upanuzi wa Bwawa la Mfili ambalo ni chanzo kikuu cha maji. Mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi 1,011,217,230 kwa mchanganuo ufuatao:-
Baada ya kukamilika kwa upanuzi wa bwawa la Mfili ujazo wa maji umeongezeka kutoka mita za ujazo 1500 za awali hadi mita za ujazo 248,067.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa