• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Wangabo afika kwenye ghala la TFC na kukuta patupu

imewekwa Tar: November 8th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametembela ghala la kuhifadhia mbolea la Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC) na kutokuta hata mfuko mmoja wa mbolea huku wakulima wakijiandaa na msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 huku mvua zikitarajiwa kuanza hivi karibuni.

Mh. Wangabo amefanya ziara fupi katika maghala kadhaa ya wafanyabiashara binafsi pamoja na makampuni yaliyopo mjini sumbawanga na kukuta shughuli za uletaji wa mbolea ukiendelea kwa maandalizi yam simu wa kilimo huku Kampuni ya Mboleaa Tanzania (TFC) ikikosa hata mfuko mmoja katika ghala lao jambo lililowashanga walioambatana na Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo.

“Tutawasiliana na viongozi wa TFC ili tuweze kujua kwanini hawaleti mbolea ya kutosha wakati hii ni kampuni ya serikali inaweza ikaleta mbolea nyingi kuliko hata hao wengine lakini badala yake “godown” (ghala) kubwa lakini hakuna kitu, nini manufaa ya TFC sasa,” Alihoji.

Awali akisoma taarifa ya kampuni hiyo msimamizi wa ghala hilo Jelio Mahenge alisema kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 207/2018 kampuni ilifanikiwa kusambaza tani 1082 na kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 kampuni imejipanga kuleta jumla ya tani 2500 kwa awamu ya kwanza.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kampuni inafanya jitihada zote za hali na mali kuhakikisha uletaji wa mbolea unatekelezeka ndani ya mwezi huu wa kumi na moja ili kuendana na msimu wa kilimo na kuleta tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla,”

Msimu wa Kilimo wa mwaka 2017/2018 Mkoa ulitumia zaidi ya tani 24,000 za Mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA) na msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 mkoa unatarajiwa kutumia zaidi ya tani 34,000 na mpaka mwanzoni mwa mwezi huu Mkoa umepokea tani 363.75 ambazo tayari zikiwa ndani ya maghala ya wafanyabiashara wa mbolea na nyingine zikiwa njiani.

Matangazo

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2019 - Rukwa October 17, 2019
  • Waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza Mkoa wa Rukwa 2018 January 05, 2018
  • Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) October 09, 2018
  • Kikao cha Road Board Mkoani Rukwa October 08, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Wagombea 1,851 wa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Mkoani Rukwa.

    November 23, 2019
  • Agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli latekelezwa kwa asilimia 100 Sumbawanga

    November 21, 2019
  • Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda awataka watumishi Rukwa kupambana na udumavu.

    November 20, 2019
  • Jaji Mkuu awaagiza viongozi wa Mahakama kusimamia usajili wa kesi mitandaoni

    November 14, 2019
  • Angalia Zote

Video

Kisa Kamili cha Mama Mjamzito Kujijeruhi tumboni chafafanuliwa na RMO Rukwa
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Regional Block, 90 Mwl. Julius Nyerere Road

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0756941328

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa