SEKTA YA MIFUGO
Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo
Zoezi la utambuzi wa mifugo kwa njia ya hereni za kieletroniki ‘Electronic Ear tags’ kutekeleza Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Wanyama Na.19 ya mwaka 2008 lilianza mwezi Agosti, 2021 na linafanyika katika Halmashauri zote. Hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2022 zoezi lilipositishwa na Serikali jumla ya ngombe 264,190 mbuzi 1,570; kondoo 457 na punda 605 walikuwa wametambuliwa.
Usimamizi wa utekelezaji wa Sheria katika Utoaji wa Huduma za Mifugo
Mwaka 2022/2023 Baraza la Veterinari Tanzania (Veterinari Council of Tanzania - VCT) kwa kushirikiana na Mkoa na Halmashauri lilifanya ukaguzi wa kawaida (Routine Inspection) katika Halmashauri. Shughuli zilizofanyika ni pamoja na usajili na ukaguzi wa wataalamu wa afya ya Wanyama na miundombinu ya Vituo vya utoaji wa huduma za afya ya Wanyama na kukagua maeneo yanayojihusisha na uuzaji wa dawa na vifaa tiba vya wanyama. Jumla ya Vituo/maduka 28 yalikaguliwa ndani mkoa na hatua kuchukuliwa kwa wale waliokutwa na makosa
Vilevile, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (Tanzania Medicines and Medical Devices Authority - TMDA) Ofisi ya Kanda – Mbeya kwa kushirikiana na Wataalamu wa Mifugo wa Manispaa ya Sumbawanga ilifanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria miongoni mwa Wadau katika maeneo yanayojihusisha na uuzaji wa dawa na vifaa tiba vya wanyama.
Ukaguzi wa miundombinu ya zao na Wadau waliokatika mnyororo wa thamani wa zao la nyama
Mwaka 2023 Bodi ya Nyama Tanzania (Tanzania Meat Board - TMB) Ofisi ya Kanda – Mbeya kwa kushirikiana na Wataalamu wa Mifugo Mkoa na Halmashauri ilifanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria miongoni mwa Wadau katika mnyororo wa thamani wa nyama na miundombinu yao katika Halmashauri ikiwa ni pamoja na hali ya usajili na viwango vya ubora wa machinjio, Minada Awali ya mifugo, wafanyabiashara wa mifugo na nyama. Miundombinu iliyokaguliwa ni minada 4, machinjio 3, magari ya kubebea nyama 4 na maduka ya nyama 54 ili kuhakikisha nyama inayozalishwa iko katika ubora na salama kwa afya ya walaji.
Ufuatiliaji Matukio ya Magonjwa ‘Field Surveillance’
Katika ufuatiliaji wa magonjwa ya wanyama, Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) ziliwasilisha jumla ya Taarifa 2,337 (Animal Diseases Surveillance Field Report) ziliwasilishwa ZVC Sumbawanga. Tathmini ya uwasilishaji taarifa za matukio ya kila wiki inaonesha kati ya Kata 97 zilizopo, jumla ya Kata zilizowasilisha (completeness) ni 74, sawa na asilimia 76 kimkoa na uwasilishaji wa Halmashauri kwa wakati muafaka (timeliness) ni asilimia 80 kimkoa.. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inaendelea kuzihimiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuatilia na kuwasilisha taarifa za matukio ya magonjwa kwa wakati muafaka.
Kinga na Udhibiti dhidi ya Magonjwa mbalimbali ya mifugo
Chanjo zilizosambazwa na TVLA kwa Halmashauri/Maduka ya Dawa
Kituo cha Kanda cha TVLA Sumbawanga kiliuza na kusambaza chanjo ndani ya Mkoa kupitia wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Halmashauri, Watoa huduma wa sekta binafsi (Maduka ya Dawa za Mifugo) na mashamba ya mifugo. Kwa mujibu wa Taarifa za TVLA, chanjo zilizouzwa na kusambazwa mwaka 2022/2023 ni:-
Aina na Dozi za Chanjo zilizouzwa na kusambazwa na TVLA
Na.
|
Aina ya Chanjo
|
Jumla ya Dozi
|
|
S19 Brucella
|
25
|
|
Chambavu - BQ
|
900
|
|
Chambavu na Kimeta (Blanthrax)
|
2,600
|
|
Homa ya Mapafu ya Mbuzi -CCPP
|
3,500
|
|
Homa ya Mapafu ya Ng’ombe - CBPP
|
6,100
|
|
Kimeta - Anthrax
|
20,000
|
|
Mdondo -Newcastle (I - 2)
|
1,641,040
|
|
Jumla
|
1,674,165
|
Chanzo: Taarifa za kila mwezi za TVLA Sumbawanga 2022/2023
Uogeshaji mifugo kudhibiti Magonjwa yanayoenezwa na Kupe
Udhibiti wadudu ambukizi na sumbufu ulifanyika katika maeneo mbalimbali kwa njia ya kuogesha mifugo. Katika kipindi cha mwaka 2021/2022 na mwaka 2022/2023 Mkoa ulipokea dawa za kuogesha mifugo jumla ya lita 2,067.5 aina ROL - DIP 330EC® - Alphacypermethrin 30g/l, Chlorpyrifos 300g/l zenye thamani ya shilingi milioni 92.97 kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuzigawa katika Halmashauri.
Pamoja na jitihada hizo za Serikali kiwango cha kuogesha mifugo kwa kutumia majosho bado kipo chini katika Halmashauri zote. Hii ni inachangiwa na matumizi yasiyoendelevu ya majosho hususan kipindi cha msimu wa kilimo kutokana na kukosekana kwa njia za mifugo kuelekea katika majosho, baadhi ya wafugaji kutokuwa tayari kuogesha mifugo yao katika majosho yaliyopo, usimamizi hafifu pamoja na kukosekana kwa majosho katika baadhi ya maeneo ya ufugaji yenye ng’ombe wengi (mtawanyiko wa majosho) hususan Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Aidha, upatikanaji wa taarifa za matumizi ya pampu za mikono upo chini ukilinganisha na hali halisi.
Katika mwaka 2022/2023 majosho 39 yalifanyakazi na kuwezesha michovyo 1,735,112 (ng’ombe 1,452,998; mbuzi 155,006; kondoo 124,373; mbwa 2,521 na punda 214).
Pia kulikuwa na minyunyizo 3,750,000 kwa kutumia pampu za mikono (ng’ombe 3,081,405; mbuzi 341,670; kondoo 247,259; nguruwe 70,218; mbwa 9,064 na punda 384). Jedwali Na. 30. Dawa (Viuatilifu) zilizotumika katika kuogesha mifugo maeneo mbalimbali ni Alphacypermethrin & Chlorpyrifos, Alphacypermethrin, Amitraz 12.5% na Cypermethrin.
Maeneo yaliotengwa kwa ajili ya malisho
Maeneo ya malisho yapo katika Halmashauri za Kalambo, Nkasi na Sumbawanga ambazo ziliandaa na kuyawasilisha katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapa chini
Maeneo ya malisho Mkoa wa Rukwa
Halmashauri
|
Kijiji
|
Ukubwa wa Eneo
|
Jina la kikundi
|
Kalambo
|
Matai Asilia
|
Ekari 5
|
Livestock and Fishfarm
|
Mbuluma
|
Ekari 5
|
Uviwakimnu
|
|
Nkasi
|
Chalatila
|
Ekari 5
|
Wafugaji
|
Paramawe B
|
Ekari 5
|
Chapakazi group
|
|
Sumbawanga DC
|
Kalambanzite
|
Ekari 5
|
Uviwakika
|
Miangalua
|
Ekari 5
|
Umoja wa Vijana Makozi
|
Mifugo ni Mingi na Ngozi ni nyingi Mkoa wa Rukwa , Ngozi iliyokaushwa kwa njia ya Chumvi
Ngozi iliyokaushwa kwa hewa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) alipotembelea kiwanda cha nyama cha SAAFI ambacho ni kiwanda pekee kilichopo Mkoa wa Rukwa.
Ombi kwa Wawekezaji
Pamoja na kuwepo kwa ng'ombe wengi kufikia nusu ya idadi ya wananchi wanaoishi Mkoa wa Rukwa bila ya kuiongelea mifugo mingine tunaona kuwa kuna uhitaji mkubwa wa uwepo wa viwanda vingi vya kusindika nyama pamoja na malighafi zinazotokana na mifugo hiyo ikiwemo ngozi, pembe, n.k.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa