Uwekezaji katika kilimo
Wakulima wengi katika Mkoa huu ni wadogo wadogo wanaolima kati ya hekta 0.5 – 2.0 na wakulima wa kati wanaoliama kati ya hekta 2.0 – 4.0. Hivi karibuni tumeanza kupata wakulima wakubwa wanaolima hekta 300 – 1,000. Kwa sasa tunao wakulima/mashamba matatu (3) ya MSIPAZI, EMPIEN na MAJINJA ambao wanalima kilimo cha kibiashara cha mashamba makubwa. Uongozi wa Mkoa tunaendelea kushirikiana nao kwa kuweka mazingira wezeshi ili wazalishe kwa tija na kuanzisha viwanda vya kusindika mazao wanayozalisha pia kuwa waelimishaji na soko kwa wakulima wanaowazunguka.
Changamoto kubwa zinazokwamisha kukua kwa sekta ya kilimo katika Mkoa wa Rukwa ni pamoja na:-
Matumizi kidogo ya pembejeo za Kilimo (mbolea, Mbegu na Viuatilifu)
Matumizi madogo ya zana za kisasa za Kilimo katika kulima, kuvuna na kuandaa mazao kabla hayapekwa katika soko.
Upungufu wa maafisa ugani kwa ajili ya kutoa elimu na stadi za Kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Matumizi madogo ya fursa kubwa ya umwagiliaji iliyopo katika mkoa.
Teknolojia za kisasa kutoka katika vituo vya utafiti kutowafikia wakulima kwa wakati.
Ukosefu wa vitendeakazi kwa Maafisa Ugani katika ngazi zote.
Mikakati ya kuendeleza sekta ya kilimo.
Mkoa umeweka mikakati ambayo inateelezwa ili kukabiliana na changamoto zinazokwamisha ukuaji wa sekta ya kilimo. Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo;
Kutumia vituo vya raslimali za kilimo katika kutoa elimu ya kilimo.
Mkoa wa Rukwa una jumla ya Vituo vya rasilimali za Kilimo 9 (Kalambo DC 1, Nkasi DC 5, Sumbawanga DC 2 na Sumbawanga MC 1). Vituo sita (6) vilivyowekewa vifaa vinatumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakulima, kupata machapisho rejea, kupata teknolojia za Kilimo kwa wakulima waliopo katika Kata.
Upatikanaji wa masoko ya mazao ya kilimo.
Soko kubwa na la uhakika la mahindi kwa wakulima wa Mkoa wetu ni kupita Wakala wa Chakula wa Taifa (NFRA)ambao hununua kwa bei ambayo hukidhi gharama za uzalishaji wa Mahindi . Kwa kuzingatia ukweli kuwa Serikali siyo soko pekee la mazao yetu inatulazimu tushirikiane na sekta binafsi, mfano TCCIA na wadau wengine kutafuta masoko ya mazao yetu ndani na nje ya nchi na kuwa tayari kushindana na wazalishaji wengine wa mahindi kwa kuongeza ubora na kupunguza gharama za uzalishaji. Aidha, katika msimu huu tumedhamiria kuwakumbusha watendaji wa Halmashauri kuvisimamia vyama vya Ushirika vilivyopo na kusimamia uanzishwaji wa vyama vipya vya ushirika wa mazao (AMCOS) .
Kuongeza matumizi ya zana za kisasa za kilimo.
Mkoa kwa kutambua kwamba tuna zana za kilimo (trekta) chache, tunaendelea na juhudi za makusudi za kuwezesha wakulima kupata zana bora za kilimo. Tulianza kuwaunganisha wakulima na shirika la SUMAJKT na sasa tutaendelea kuwaunganisha wakulima na NDC na Agricom ili waweze kukopa matrekta . Mkoa utaendelea kuhakikisha kuwa zana zilizopo katika mkoa zinatumika ipasavyo katika kuongeza tija katika kilimo.
Kuboresha kilimo cha umwagiliaji
Mkoa utaendelea kutoa elimu juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji katika skimu za umwagiliaji zilizopo na kuwachukulia sheria baada ya kuwaelimisha kwa wale watakaobainika kuhushika na uharibifu wa mazingira. Tutaendelea kufanya kaguzi wa hali ya miundombinu ya umwagiliaji kabla na baada ya msimu wa mvua ili kubaini uharibifu uliopo katika miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kutoa elimu kwa umoja wa umwagiliaji juu ya umuhimu wa kuchangia katika kukarabati miundombinu ya umwagiliaji. Mkoa unaendelea kuwahamasisha wakulima kujiunga pamoja na kujenga baadhi ya miundombinu ya umwagiliaji kwa kutumia guvu zao.
Matumizi madogo ya pembejeo.
Mkoa unaendelea kushirikiana na TFRA kuhakikisha kuwa Mbolea inapatikana katika Mkoa kupitia mfumo unaojulikana kama ‘Bulk Procurement System’
Mfumo huu unasimamiwa na sheria ya usimamizi wa mbolea namba 9 ya mwaka 2009, kifungu cha 51 na kanuni za Mwaka 2017. Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority-TFRA) wamepewa kazi ya kusimamia upatikana na usimamizi wa sheria ya mbolea katika Nchi.
Aidha Mkoa unaendelea kushirikiana na Mamlaka ya udhibiti wa ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) katika kuhakikisha kuwa mbegu zinazo wafikia wakulima ni zile zenye ubora. Tunaendelea kusisitiza kuwa wakulima wajiunge pamoja na kuangiza mbolea na mbegu moja kwa moja kwa wazalishaji ili kuondokana na uchakachuaji na kupunguza gharama.
Upungufu wa Maafisa Ugani.
Serikali inaendelea kuajiri watumishi ikiwemo wale wa kilimo ili kukidhi mahitaji ya maafisa hao. Vile vile tumepokea maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu ya kupunguza watumishi waliopo makao makuu ya Halmashauri na kuwapangia maeneo ya kata na vijiji ambako kuna mahitaji makubwa ya watumishi hao. Vile vile Mkoa unashirikiana na sekta binafsi katika kutoa huduma za ugani kwa wakulima waliopo katika Halmashauri zetu.
Matumizi ya zana za kilimo.
Matumizi ya zana za kilimo zinazokokotwa na wanyamakazi (Maksai) Mkoa ni asilimia 74, matumizi ya matrekta ni asilimia 4 na matumizi ya jembe la mkono ni asilimia 22. Mkoa una jumla ya matrekta makubwa yapatayo 121, madogo 114, combine harvester 11 na maksai 105,855 kama inavyonekana katika jedwali hapo chini.
|
|
|
|
|
Sumbawanga (M)
|
|
|
|
|
Sumbawanga (W)
|
|
|
|
|
Nkasi
|
|
|
|
|
Kalambo
|
|
|
|
|
Jumla
|
|
|
|
|
Mahindi ni miongoni mwa Zao Kubwa linalolimwa kwa wingi Mkoa wa Rukwa
Kilimo cha Alizeti nacho kinapewa kipaumbele katika mkoa wa Rukwa
Maboga nayo yamekuwa ni biashara kubwa katika Mkoa wa Rukwa
Ngano ni miongoni mwa mazao yanayoshamiri na kulimwa kwa wingi Mkoani Rukwa
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa