SEKTA YA MIFUGO
Wakaguzi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (Tanzania Medicines and Medical Devices Authority - TMDA) walifanya ukaguzi Maalum katika maduka yanayouza dawa za mifugo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Mji wa Namanyere katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi tarehe 15 na 16 Oktoba, 2019. Aidha, Mkaguzi kutoka Ofisi ya Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), Dodoma alifika na kufanya ukaguzi wa kawaida katika baadhi ya maeneo kuanzia tarehe 17.10.2019 hadi 20.10.2019 kwa kushirikiana na Daktari wa Mifugo - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wataalamu wa Mifugo wa Halmashauri husika (Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga, Halmashauri za Wilaya ya Kalambo na Nkasi).
Mkaguzi wa Nyanda za Juu Kusini - Ofisi ya Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), Dodoma alifika na kufanya ukaguzi wa kawaida katika baadhi ya maeneo kuanzia tarehe 17.2.2020 hadi 20.2.2020 kwa kushirikiana na Wataalamu wa Mifugo wa Halmashauri husika (Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na Kalambo).
Matokeo ya Kaguzi hizo, Jumla ya maeneo 26 yalikaguliwa ambapo, Dawa aina ya VETOXY 20®, BIOSOL® , ALBENDEX®, LEVAZOLE® , OXYZASH Bolus® na EWP Topical Application ambazo hazikuwa na usajili wa TMDA na dawa aina ya PEN & STREP® ya kampuni ya Norbrook na PEN-STREP 20/25® ya kampuni ya Farvet zilizokutwa hazijahifadhiwa katika jokofu (nyuzi joto 2O C – 8O C) ziliondolewa katika soko (madukani), wamiliki 9 walitozwa faini jumla Sh. 4,700,000/= kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Veterinari zinazosimamiwa na VCT, wawili walilipa ada Sh. 280,000/=, wawili (10) walionywa waache biashara ya kuuza dawa za mifugo kwa hiari yao hadi hapo watakapokamilisha taratibu za usajili wa maduka/vituo vyao katika Baraza la Veterinari - VCT na maduka matano (5) yalifungwa yalifungwa na VCT kutokana na kukiukwa Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji wa Maduka ya Dawa za Mifugo. Aidha, Mkaguzi alipopita mwezi Februari, 2020 Ukaguzi haukufanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri kuomba zoezi hilo liahirishwe kwa muda wa mwezi mmoja katika eneo lake ili aweze kuongea na wamiliki wa maduka yaliyopo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na ZVC Sumbawanga na wadau wengine (Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nkasi, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na Meneja wa Pori la Akiba Lwafi) ilifanya ufuatiliaji wa ng’ombe 702 waliokuwa wameingizwa katika Pori la Akiba la Lwafi kinyume na Sheria na kufanikiwa kusuluhisha mgogoro huo. Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na wahusika kulipa faini ya shilingi 13,960,000 kwa ng’ombe 698 waliokuwa wamebaki baada ya ndama 4 kufa.
Serikali ilifanikiwa kukamata Wadau kumi na nne (14) na mayai 56,220 (trei 1,874) yaliyoingizwa bila Vibali na kuwatoza faini wadau hao jumla ya shilingi 3,380,000/= aidha, kati ya trei hizo zilizokamatwa jumla ya mayai 10,920 (trei 364) yanayosadikiwa kuingizwa kutoka Zambia kupitia Tunduma yaliteketezwa.
Pamoja na hatua hizo, Wadau walipewa elimu ya kuzingatia Sheria na Kanuni katika usafirishaji wa mayai.
Katika ufuatiliaji wa magonjwa ya wanyama, Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) ziliwasilisha jumla ya Taarifa 845 (Animal Diseases Surveillance Field Report) ziliwasilishwa ZVC Sumbawanga, ambapo katika utaratibu wa kila wiki taarifa 799 na utaratibu wa EMAi taarifa 46. Kiwango cha uwasilishaji taarifa za kila wiki kutoka ngazi ya Vijiji/Kata kipo chini sana. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inaendelea kuzihimiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuatilia na kuwasilisha taarifa za matukio ya magonjwa kwa wakati muafaka.
Kituo cha Kanda cha TVLA Sumbawanga kiliuza na kusambaza chanjo ndani ya Mkoa kupitia wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Halmashauri, Watoa huduma wa sekta binafsi (Maduka ya Dawa za Mifugo) na mashamba ya mifugo. Kwa mujibu wa Taarifa za TVLA, chanjo zilizouzwa na kusambazwa mwaka 2019/2020 ni:-
Aina na Dozi za Chanjo zilizouzwa na kusambazwa na TVLA
Na.
|
Aina ya Chanjo
|
Jumla ya Dozi |
|
Mdondo -Newcastle (I - 2)
|
1,878,500 |
|
Homa ya Mapafu ya Ng’ombe - CBPP
|
5,000 |
|
Chambavu na Kimeta (Blanthrax)
|
2,850 |
|
Chambavu
|
3,750 |
|
S19 Brucella
|
250 |
|
Jumla
|
1,890,350 |
Chanzo: Taarifa za kila mwezi za TVLA Sumbawanga 2019/2020
Udhibiti wadudu ambukizi na sumbufu ulifanyika katika maeneo mbalimbali kwa njia ya kuogesha mifugo. Katika kipindi cha mwaka 2019/2020, mkoa ulipokea viuatilifu vya kuogesha mifugo jumla ya lita 617 aina ya TikTik Amitraz 12.5% na lita 188 aina ya Paranex ‘Alphacypermethrin’ kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuzigawa katika Halmashauri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilifanya hamasa na ufuatiliaji wa utekelezaji kampeni ya kukarabati au kujenga majosho na kuogesha mifugo. Ambapo katika kipindi cha mwaka 2019/2020 majosho yaliyokarabatiwa ni 12 (majosho 8 kwa ufadhili wa Wizara na 4 kwa fedha za Halmashauri) na josho 1 limejengwa na wafugaji binafsi. Hivyo kumekuwa na ongezeko la majosho mazima kutoka 53 hadi 61 na majosho yaliyofanyakazi kutoka 40 hadi 56 mwaka 2019/2020 ukilinganisha na mwaka 2018/2019.
Pamoja na jitihada hizo za Serikali kiwango cha kuogesha mifugo kwa kutumia majosho bado kipo chini katika Halmashauri zote. Hii ni inachangiwa na matumizi yasiyoendelevu ya majosho hususan kipindi cha msimu wa kilimo kutokana na kukosekana kwa njia za mifugo kuelekea katika majosho, baadhi ya wafugaji kutokuwa tayari kuogesha mifugo yao katika majosho yaliyopo, usimamizi hafifu pamoja na kukosekana kwa majosho katika baadhi ya maeneo ya ufugaji yenye ng’ombe wengi (mtawanyiko wa majosho) hususan Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Aidha, upatikanaji wa taarifa za matumizi ya pampu za mikono upo chini ukilinganisha na hali halisi.
Katika mwaka 2019/2020 majosho 56 yalifanyakazi na kuwezesha michovyo 1,804,507 (1,512,599 ya ng’ombe; 238,877 ya mbuzi; 51,567 ya kondoo na 1,879 ya mbwa). Jedwali Na. 30 na 32.
Pia kulikuwa na minyunyizo 1,228,365 kwa kutumia pampu za mikono (946,864 ya ng’ombe; 180,609 ya mbuzi; 61,725 ya kondoo; 32,144 ya nguruwe na 7,023 ya mbwa) Jedwali Na. 30. Dawa (Viuatilifu) zilizotumika katika kuogesha mifugo maeneo mbalimbali ni Amitraz 12.5%, Alphacypermethrin na Cypermethrin.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa