Mkoa wa Rukwa ulianzishwa mwaka 1974 kwa kumega sehemu ya Mkoa wa Tabora (Mpanda) na Mbeya (Sumbawanga). Mnamo mwezi Julai 2010 Serikali ya Awamu ya Nne iliridhia kugawanywa kwa Mkoa wa Rukwa na kuanzishwa kwa Mkoa mpya wa Katavi.
Jiografia ya Mkoa
Mkoa wa Rukwa upo kati ya Latitudo 70 – 90 Kusini ya Ikweta na Longitudo 30 – 320 Mashariki ya Grinwichi. Mkoa huu unapakana na Mikoa ya Katavi upande wa Kaskazini na Songwe upande wa Kusini Mashariki; Aidha, unapakana na nchi za Zambia upande wa Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa Magharibi. Eneo la juu sana katika Mkoa wa Rukwa linapatikana Malonje katika Nyanda za juu za Ufipa ambalo ni Mita 2,461 Juu ya Usawa wa Bahari na eneo la chini zaidi ni Ziwa Tanganyika lenye Mita 773 Juu ya Usawa wa Bahari.
Eneo la Mkoa
Mkoa huu una eneo la kilomita za mraba 27,765, kati ya hizo Kilomita za mraba 21,160 (76.21%) ni za nchi kavu na Kilomita za mraba 6,605 (23.79%) ni za maji kama ilivyoainishwa katika Jedwali
Eneo Mkoa wa Rukwa mwaka 2017
Wilaya
|
Halmashauri ya Wilaya/ Manispaa
|
Eneo Km. za mraba
|
Eneo la Ardhi.
|
Eneo la Maji.
|
||
Km2
|
%
|
Km2
|
%
|
|||
S’wanga
|
S’wanga MC
|
1,329
|
1,329
|
100.0
|
0
|
0
|
S’wanga DC
|
8,871
|
8,203
|
92.5
|
668
|
7.5
|
|
Nkasi
|
Nkasi
|
13,124
|
9,375
|
71.4
|
3,749
|
28.6
|
Kalambo
|
Kalambo
|
4,441
|
3,937
|
88.7
|
504
|
11.3
|
Jumla
|
|
27,765
|
21,160
|
76.21
|
6,605
|
23.79
|
Muundo wa Mkoa Kiutawala
Mkoa wa Rukwa umegawanyika katika Wilaya tatu (3), zenye Halmashauri nne (4), Tarafa 16, Kata 97, Vijiji 339 Vitongoji 1,825 Kaya 185,076 na Mitaa 167. Wilaya hizo ni Sumbawanga, Kalambo na Nkasi. Mkoa unajumuisha Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Nkasi na Kalambo. Aidha, ndani ya Mkoa kuna Mamlaka za Miji Midogo miwili ambazo ni Namanyere Wilaya ya Nkasi na Laela Wilaya ya Sumbawanga. Yapo majimbo matano (5) ya Uchaguzi ambayo ni: Sumbawanga Mjini na Kwela – Wilaya ya Sumbawanga; Kalambo – Wilaya ya Kalambo; Nkasi Kusini na Nkasi Kaskazini – Wilaya ya Nkasi.
Eneo la Muundo wa Utawala Mkoa wa Rukwa 2022
Wilaya
|
Halmashauri
|
Eneo Km. Za mraba
|
IDADI YA
|
|||||
Tarafa
|
Kata
|
Vijiji
|
Vitongoji
|
Mitaa
|
Majimbo ya Uchaguzi
|
|||
S’wanga
|
S’wanga MC
|
1,329
|
2
|
19
|
24
|
176
|
167
|
1
|
S’wanga DC
|
8,871
|
4
|
27
|
114
|
494
|
0
|
1
|
|
Nkasi
|
Nkasi
|
13,124
|
5
|
28
|
90
|
725
|
0
|
2
|
Kalambo
|
Kalambo
|
4,441
|
5
|
23
|
111
|
422
|
0
|
1
|
Jumla
|
|
27,765
|
16
|
97
|
339
|
1817
|
167
|
5
|
Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2022, Mkoa wa Rukwa ulikuwa na Wakazi wapatao 1,540,519 ambapo Wanawake ni 797,400 na Wanaume ni 743,119. Mkoa pia unazo Kaya 330,013 na wastani wa wakazi kwa Kaya moja ni watano (6.9). Ongezeko hili ni sawa na wastani wa asilimia 3.2% kwa Mwaka kama ilivyo katika jedwali
Idadi ya Wakazi Kiwilaya kwa Mwaka 2022
|
|||||
HALMASHAURI
|
IDADI
|
WAKAZI KWA KAYA
|
|||
ME
|
KE
|
JUMLA
|
KAYA
|
WASTANI
|
|
Sumbawanga MC
|
303,986
|
109,059
|
209,793
|
70,334
|
4.8
|
Sumbawanga DC
|
494,330
|
156,784
|
305,846
|
105,551
|
5.0
|
Nkasi DC
|
425,420
|
144,159
|
281,200
|
84,903
|
5.3
|
Kalambo DC
|
316,783
|
107,226
|
207,700
|
69,225
|
4.9
|
Jumla
|
743,119
|
797,400
|
1,540,519
|
330,013
|
6.9
|
Hali ya hewa
Mkoa wa Rukwa una hali ya hewa ya Kitropiki ambapo wastani wa joto ni Sentigredi 13 katika baadhi ya maeneo kwa miezi ya Juni na Julai hadi Sentigredi 27 kwa miezi yenye joto jingi ya Oktoba na Desemba. Mkoa umebahatika kuwa na mvua za kuaminika kwa miaka mingi; mvua za Mkoa huu ni wastani wa milimita 850 kwa mwaka zikinyesha kuanzia mwezi wa Novemba – Mei. Kiangazi huanza mwezi Juni mara baada ya majira ya mvua hadi mwezi wa Oktoba.
Shughuli za Kiuchumi
Kiuchumi, wakazi wa Mkoa wa Rukwa wanajishughulisha na, Kilimo cha mazao ya chakula na biashara, ufugaji, sekta ya utalii, madini, uvuvi, viwanda vidogo pamoja na biashara ndogondogo. Shughuli kuu ya Kiuchumi ni Kilimo, ambapo mazao ya chakula yanayolimwa kwa wingi ni Mahindi, Mpunga, Viazi vitamu, Viazi mviringo, Mihogo, Maharage na Ulezi. Mazao ya biashara yanayolimwa kwa wingi ni Alizeti, Ngano, Ufuta na Michikichi. Aidha, ziada ya Mazao ya chakula kama Mahindi, Mpunga, Maharage, Ulezi, Ngano, Shayiri na Karanga hutumika pia kama mazao ya biashara. Ufugaji unabaki kuwa shughuli kuu muhimu ya pili ya uchumi katika Mkoa wa Rukwa. Mifugo inayofugwa kwa wingi ni Ng’ombe, Mbuzi, Nguruwe, Kondoo, Punda na Kuku.
Pato la Mkoa wa Rukwa
Kwa upande wa Pato la Taifa Mkoa wa Rukwa unakadiriwa kuwa na Pato la Taifa (GDP) kwa bei ya sasa ya Tshs. trilioni 4.5 kulingana na ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS, 2019) iliyochangia takriban asilimia 6.1 ya Pato la Taifa. Mkoa pia una pato la mtaji la 2,341,860.00 ikishika nafasi ya 16 kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara
.
Historia ya Viongozi kwa Mkoa wa Rukwa
Orodha ya Wakuu wa Mkoa tangu mkoa ulipoanzishwa.
Na
|
Jina Kamili
|
Tarehe aliyoanza
|
Tarehe Aliyoondoka
|
1.
|
Mr. M.G. Baruti
|
1, Januari 1974
|
21, Februari 1983
|
2.
|
Mr. E.S. Mnyawami
|
22, Februari 1983
|
5, Juni 1984
|
3.
|
Mej. Gen. T. Kiwelu
|
6, Juni 1984
|
14, Novemba 1988
|
4.
|
Capt. P.N. Kafanabo
|
15, Novemba 1988
|
9, Disemba 1990
|
5.
|
Dr. K.M. Kiwanuka
|
10, Disemba 1990
|
8, Septemba 1991
|
6.
|
Mr. A.S. Aljabri
|
9, Septemba 1991
|
5, Novemba 1993
|
7.
|
Mr. C.M. Mzindakaya
|
6, Novemba 19993
|
30, Disemba 1995
|
8.
|
Mej. S. Nswima
|
31, Disemba 1995
|
10, Disemba 1997
|
9.
|
Capt. Jaka M. Mwambi
|
11, Disemba 1997
|
7, Februari 2003
|
10.
|
Capt. G.H. Mkuchika
|
8, Februari 2003
|
20, Agosti 2005
|
11.
|
Daniel Ole Njoolay
|
6, Februari 2006
|
15, Septemba 2011
|
12.
|
Eng. Stella Martin Manyanya
|
16, Septemba 2011
|
30, Agosti 2015
|
13.
|
Magalula Said Magalula
|
31, Agosti 2015
|
13, Machi 2016
|
14.
|
Zelote Stephen Zelote
|
13, Machi 2016
|
26, Oktoba 2017
|
15.
|
Joachim leonard Wangabo
|
26, Oktoba 2017
|
15, Mei 2021
|
16.
|
Joseph Mkirikiti
|
15, Mei 2021
|
28, Julai 2022
|
17
|
Queen C. Sendiga
|
28, Julai 2022
|
23, Mei 2023
|
18
|
Charles Makongoro Nyerere
|
23, Mei 2023
|
|
Orodha ya Makatibu Tawala wa Mkoa tangu kuanzishwa kwa Mkoa
Namba
|
Jina
|
Tangu
|
Mpaka
|
1.
|
J. Matiko
|
1.1.1974
|
29.3.1975
|
2.
|
D.F.P Ringo
|
30.3.1975
|
18.8.1976
|
3.
|
R.S. Lukindo
|
19.8.1976
|
6.1.1980
|
4.
|
S.K. Masinde
|
7.1.1980
|
2.1.1984
|
5.
|
C.T. Kisanji
|
2.1.1984
|
17.11.1985
|
6.
|
T.N. Machume
|
18.11.1985
|
16.2.1989
|
7.
|
A.A.K. Mwasajone
|
17.2.1989
|
17.2.1994
|
8.
|
P.A. M Chikira
|
20.5.1995
|
14.2.1997
|
9.
|
W. Ngirwa
|
15.2.1997
|
15.11.1998
|
10.
|
H.N.M. Kachechele
|
16.11.1998
|
3.4.2006
|
11.
|
Innocent Mwenda
|
4.4.2006
|
7.7.2009
|
12.
|
Salum .M.Chima
|
25.1.2010
|
18.1.2014
|
13.
|
Smythies E. Pangisa
|
18.1.2014
|
29.2.2016
|
14.
|
Tixon Tuyangine Nzunda
|
9.9.2016
|
23.5.2017
|
15.
|
Bernard Mtandi Makali
|
23.5.2017
|
05.06.2021
|
16.
|
Denis Isdory Bandisa
|
05.06.2021
|
28.07.2022
|
17
|
Rashid K. Mchatta
|
28.07.2022
|
16.03.2023
|
18.
|
Gerald M. Kusaya
|
16.03.2023
|
09.03.2024 |
19. | Msalika R. Makungu | 09.03.2024 |
|
|
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa