SEKTA YA AFYA, LISHE NA USTAWI WA JAMII
HALI YA WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA KATIKA MKOA
Mkoa una jumla ya watumishi 1980 kati ya watumishi 4,523 wanaohitajika hivyo kufanya upungufu wa watumishi 2537 kama ilivyo katika Jedwali Na.1. hapa chini:-
Jedwali Na.1 .Mchanganuo wa watumishi wa Afya
Mamlaka
|
Mahitaji |
Waliopo |
Upungufu/ Ziada
|
HM Sumbawanga
|
698 |
370 |
328(47%) |
HW Sumbawanga
|
1207 |
429 |
778(64%) |
HW Nkasi
|
920 |
433 |
487(53%) |
HW Kalambo
|
1232 |
428 |
804(65%) |
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
|
466 |
320 |
146(31%) |
Jumla (Mkoa)
|
4523 |
1980 |
2543(56%) |
Jedwali Na.2.Vituo vya kutolea huduma za afya kwa ujumla
Ngazi ya Kituo |
Umiliki |
Jumla
|
|||||
RRH
|
Halmashauri
|
Binafsi
|
FBO
|
Taasisi za Serikali
|
Taasisi nyingine
|
||
Hospitali
|
1 |
4 |
0 |
2 |
0 |
0 |
7 |
Kituo cha Afya
|
0 |
16 |
1 |
8 |
0 |
0 |
25 |
Zahanati
|
0 |
188 |
15 |
9 |
7 |
0 |
219 |
Kliniki Maalum
|
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Jumla (Mkoa)
|
1 |
240 |
18 |
20 |
6 |
0 |
251 |
2.0 Taarifa Ya Hali Miradi Ya Miundombinu Ya Kutolea Huduma Za Afya Katika Mkoa.
2.1. Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri.
Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri unaendelea katika Halmashauri nne ndani ya Mkoa. Halmashauri zinazotekeleza ujenzi wa Hospitali ni Halmashauri za Wilaya za Nkasi, Kalambo, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ambapo hadi kufikia Juni, 2023 jumla ya Shilingi 12,897,500.00 zilikuwa zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hizo ambapo kiasi cha Shilingi 12,700,000,000 zikitoka Serikali Kuu na Kiasi cha shilingi 301,000,000.00 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri, kama inavyoonekana kwenye jedwali Na3
Jedwali Na.3 .Mapokezi ya Fedha za ujenzi wa Hospitali za Halmashauri
Na
|
Halmashauri
|
Fedha iliyotolewa (Serikali Kuu) |
Fedha iliyotolewa (Mapato ya Ndani) |
Jumla ya fedha iliyotolewa |
1
|
Sumbawanga MC
|
2,550,000,000 |
11,500,000.00 |
2,561,500,000 |
2
|
Sumbawanga DC
|
3,400,000,000 |
0 |
3,400,000,000 |
3
|
Nkasi DC
|
3,400,000,000 |
146,000,000 |
3,546,000,000 |
4
|
Kalambo DC
|
3,350,000,000 |
40,000,000 |
3,390,000,000 |
|
Jumla
|
12,700,000,000 |
301,000,000 |
12,897,500,000 |
2.2 Ujenzi wa vituo vya Afya.
Hadi kufikia Septemba, 2023 Mkoa umetekeleza ujenzi wa vituo vya afya 21 ambavyo vimepokea jumla ya shilingi 9,703,374,500 Kati ya fedha hizo shilingi 528,374,000 ni fedha za mapato ya ndani, shilingi 8,900,000,000 ni fedha kutoka Serikali kuu, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.
Jedwali Na. 4. Fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa vituo vya Afya
Na
|
Halmashauri
|
Fedha iliyotolewa (Serikali Kuu) |
Fedha iliyotolewa (Mapato ya Ndani) |
Jumla ya fedha iliyotolewa |
1
|
Sumbawanga MC
|
1,800,000,000 |
76,374,500 |
1,876,374,500 |
2
|
Sumbawanga DC
|
1,400,000,000 |
580,000,000 |
1,980,000,000 |
3
|
Nkasi DC
|
3,300,000,000 |
47,000,000 |
3,347,000,000 |
4
|
Kalambo DC
|
2,400,000,000 |
100,000,000 |
2,500,000,000 |
|
Jumla
|
8,900,000,000 |
803,374,500 |
9,703,374,500 |
Mkoa umejenga jumla ya vituo vya Afya 21 kupitia fedha zilizokelewa kati ya hivyo vituo 7vimenza kutoa huduma za upasuaji wa dharura, 17 vinatoa huduma kwa wagonjwa wan je na Vituo vya Afya 4 bado haviajaanza kutoa huduma. Hii imesaidia kuboresha huduma pamoja na kupunguza vifo vya akina mama na Watoto wachanga vitokanavyo na uzazi
2.3. Ukamilishaji wa maboma ya Zahanati.
Kwa kipindi cha kuishia Septemba, 2023 Mkoa umepokea jumla ya shilingi 1,597,537,465 kwa ajili ya umaliziaji wa maboma 31 ya Zahanati kwenye halmashauri zote nne za Mkoa wa Rukwa, Kati ya fedha hizo, shilingi 1,522,537,465 ni fedha za Serikali kuu na shilingi 75,000,000 ni fedha za Mapato ya ndani. Mchanganuo wa fedha za ukamilishaji wa maboma ya zahanati umeonyeshwa kwenye Jedwali Na.5
Jedwali Na.5.Ujenzi wa Maboma katika Halmashauri
Na
|
Halmashauri
|
Fedha iliyotolewa (Serikali Kuu) |
Fedha iliyotolewa (Mapato ya Ndani) |
Jumla ya fedha iliyotolewa |
1
|
Sumbawanga MC
|
250,000,000 |
25,000,000 |
275,000,000 |
2
|
Sumbawanga DC
|
304,209,079 |
0 |
304,209,079 |
3
|
Nkasi DC
|
664,219,307 |
50,000,000 |
714,219,307 |
4
|
Kalambo DC
|
304,109,079 |
0 |
304,109,079 |
|
Jumla
|
1,522,537,465 |
75,000,000 |
1,597,537,465 |
Hadi sasa Mkoa umepokea jumla ya shilingi 2,432,293,134 kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya huduma endelevu za maji na usafi wa mazingira vijijini (The Sustainable Rural Water Supply and Sanitation Program-SRWSS). Fedha hizo zimepokelewa kwa awamu tatu kati ya 2019/2020, 2020/2021 na 2022/2023. Fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji na usafi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, shughuli za uratibu wa program ngazi ya Mkoa na Halmashauri na uhamasishaji wa usafi wa mazingira kwenye jamii. Hadi sasa jumla ya vituo 61 vya kutolea huduma za afya vimepatiwa fedha za ujenzi wa miundombinu ya Maji na usafi wa mazingira ndani ya Mkoa. Mchanganuo wa fedha zilizopokelewa umeonyeshwa kwenye jedwali Na.6
Jedwali Na.6.Fedha za utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa maji na usafi wa mazingira kwenye Vituo vya kutolea huduma za Afya
Halmashauri
|
Fedha za Awali (2019/2020) |
Mavuno ya m waka wa kwanza |
Mavuno ya mwaka wa pili |
JUMLA |
(2020/2021) |
(2021/2022) |
|||
Kalambo DC
|
272,830,000 |
365,920,000 |
276,462,586 |
915,212,586 |
Nkasi DC
|
272,830,000 |
218,080,000 |
456,140,548 |
947,050,548 |
Sumbawanga DC
|
272,830,000 |
287,200,000 |
10,000,000 |
570,030,000 |
Jumla
|
818,490,000 |
871,200,000 |
742,603,134 |
2,432,293,134 |
2.5. Ujenzi wa Nyumba za Watumishi
Mkoa pia ulipokea jumla ya shilingi. 270,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba tatu za watumishi (three in one) kwenye Halmashauri tatu za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga kupitia mpango wa maendeleo ya ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19.
2.6. Mapokezi ya Fedha za Miradi kwa Mwaka 2023/2024
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 Mkoa umepokea kiasi cha fedha shilingi bilioni 3,820,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma kupitia vyanzo vifuatavyo;- kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.
Jedwali Na.7. Mapokezi ya Fedha za Miradi kwa Mwaka wa fedha 2023
FEDHA ZA MIRADI ZILIZOPOKELEWA HALMASHAURI KWA MWAKA 2023/2024 |
JUMLA |
|||||
VOTE NAME |
UJENZI WA HOSPITALI ZA WILAYA |
ORODHA YA VITUO VYA AFYA 318 VINAVYOJENGWA VINAVYOHITAJI VIFAA |
UJENZI/UKAMILISHAJI WA VITUO VYA AFYA |
UKAMILISHAJI WA ZAHANATI |
ORODHA YA ZANAHATI 564 ZINAZOHITAJI VIFAA |
|
RukwaRegion |
|
|
|
|
|
|
Sumbawanga MC |
1,070,000,000 |
300,000,000 |
500,000,000 |
50,000,000 |
100,000,000 |
2,020,000,000 |
Sumbawanga DC |
- |
- |
- |
100,000,000 |
- |
100,000,000 |
Nkasi DC |
- |
600,000,000 |
- |
200,000,000 |
100,000,000 |
900,000,000 |
Kalambo DC |
- |
300,000,000 |
- |
400,000,000 |
100,000,000 |
800,000,000 |
|
1,070,000,000 |
1,200,000,000 |
500,000,000 |
750,000,000 |
300,000,000 |
3,820,000,000 |
kiasi cha fedha shilingi bilioni 3,820,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na ukamilishaji wa maboma ya Zahanati kwa mchanganuo ufuatao;-
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imepokea kiasi cha fedha Jumla ya shilingi bilioni 2,020,000,000/= ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1,070,000,000.00 kwa kuendeleza ujenzi Hospitali ya Manispaa Sumbawanga, milioni 500,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Senga na Sumbawanga na kiasi cha fedha shilingi milioni 50,000,000.00 umaliziaji wa ujenzi wa Zahanati ya Milanzi. Lakini pia Kiasi cha shilingi milioni 400,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Zahanati Mpya na Vituo vya Afya.
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi imepokea kiasi cha fedha shilingi milioni 900,000,000.00, ambapo kiasi cha fedha shilingi milioni milioni 700,000,000.00 ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na shilingi milioni milioni 200,000,000.00 kwa ajili ukamilishaji wa maboma ya Zahanati 4. Mchakato wa manunuzi unaendelea.
Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga imepokea kiasi cha fedha kiasi cha shilingi 100,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa Zahanati 2.
Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kiasi cha fedha shilingi milioni 800,000,000, ampapo shilingi milioni 400,000,000.00 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati 8 na kiasi cha fedha shilingi milioni 400,000,000 kwa ajili ya vifaa tiba ngazi ya Vituo vya Afya na Zahanati.
3.0 HALI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA
3.1. Huduma za kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI
3.2.1. Hali ya Maambuki ya VVU katika Mkoa
Kutokana na ripoti ya utafiti wa kitaifa wa mwaka 2016/2017 “Tanzania HIV Impact Survey” (THIS-2016/2017), kiwango cha maambukizi ya VVU (UKIMWI) Kitaifa kimeshuka kutoka 5.1% had 4.7%, kiwango cha kuwabaini watu wanaokadiriwa kuishi na VVU nchini ni 52.2%, kiwango cha kuwaanzishia dawa za kufubaza makali ya VVU watu waliotambuliwa kuwa na VVU ni 90.9%, na kupungua kwa kiwango cha VVU kwenye damu (Viral Suppression) ni 87.7%. Matokeo ya utafiti huu pia yameonyesha kuwa kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kwa Mikoa ya Nyanda za juu kusini ni wastani wa 4.7% sawa na wastani wa kitaifa na kiwango cha maabukizi kwa Mkoa wa Rukwa ni 4.4% ambacho kimepungua kutoka 6.2% (2011/2012)
Kupitia malengo na mikakati ya Kitaifa na Kimataifa ambayo ndiyo dira kuelekea mafanikio katika vita hii. Miongoni mwa Mikakati hiyo ni pamoja na;- Mkakati wa Dunia wa kutokomeza janga la UKIMWI kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI (United Nations against AIDS-UNAIDS) unaolenga kufikia 95-95-95 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025 na Mpango wa Taifa wa kufikia sifuri 3 ifikapo mwaka 2030
Malengo ya tisini na tano tatu (95, 95, 95) ifikapo Disemba, 2025: Hadi kufikia Septemba, 2023 Mkoa umefanikiwa kutekeleza malengo haya kama ifuatavyo;-
3.2.3.HUDUMA ZA KINGA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI
Mkoa kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo unasimamia miongozo ya utekelezaji wa shughuli mbali mbali za kinga dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI kama ifuatavyo:-
Huduma za unasihi na upimaji wa VVU
Tohara ya hiari ya Kitabibu kwa wanaume (VMMC).
Matumizi ya Kondomu
Huduma za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT)
Huduma za uzazi wa mpango
Huduma za kifua kikuu na UKIMWI (TB/HIV)
Huduma za Tiba na Matunzo (CTC)
Huduma ya uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya kikazi (CECAP)
3.2.4. Mafanikio kwenye eneo la Huduma za Kupambana na VVU/UKIMWI
Kupitia ufadhili wa shirika la HJFMRI katika utekelezaji wa afua za kupambana na UKIMWI, Mkoa umepata mafanikio yafuatayo; -
3.2.5.Changamoto katika eneo la huduma za Kupambana na VVU/UKIMWI
Pamoja na mafanikio yaliyopatikana, zipo changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza katika kutekeleza shughuli za kupambana na VVU/UKIMWI kama ifuatavyo; -.
3.2.6. Mikakati Ya Mkoa dhidi ya Janga la VVU/UKIMWI
Katika kipindi cha kuandaa mikakati ya Mkoa, tunapaswa kutambua uwepo wa malengo na Mikakati ya Kitaifa na Kimataifa ambayo ndiyo dira kuelekea mafanikio katika vita hii. Miongoni mwa Mikakati hiyo ni pamoja na;-
Pamoja na mikakati hiyo, Mkoa umejiwekea mikakati ifuatayo katika kupambana na janga la UKIMWI.
Kubaini wahisiwa wa virusi vya UKIMWI hasa wanaume na mabinti ambao hawajapata huduma za upimaji.
Kurudisha watoto kwenye huduma za dawa kwa 98% (98% Retention rate).
Kuongeza kiwango cha kufubaaa kwa virusi kwa Watoto kwa kuhakikisha kuwa Watoto wanapata dawa sahihi za kufubaza virusi vya UKIMWI. (Pediatric formulations)
Kutoa dawa kinga kwa makundi maalumu wakiwemo wanawake wanaonyonyesha (PrEP & PEP).
Kuongeza utoaji wa dawa za ARV kwa utaratibu wa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja (Multi Month Scripting-MMS) ambapo kwa sasa tumeruhusiwa kutoa dawa za miezi sita (6).
Upimaji wa VVU kwa watu wa karibu na mteja aliyetambulika kuwa na maambukizi ya VVU na kusajiliwa kwenye mfumo wa tiba na malezi (Index Case Testing)
Kuhakikisha wateja wote waliosajiliwa kwenye huduma za tiba na malezi wanabakia kwenye huduma hizo (Retention)
Kuhakikisha wateja wote waliosajiliwa kwenye huduma za tiba na malezi wanaostahili kupewa dawa kinga ya Kifua Kikuu, wanapatiwa dawa hizo (TPT)
Kuongeza vituo vya huduma ya tohara (static sites) kwa kila Halmashauri kwa 10% kila mwaka.
3.3. HALI YA HUDUMA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA
3.3.1. HALI YA KIFUA KIKUU KATIKA MKOA
Mkoa umepiga hatua kadhaa katika kuboresha huduma za Kifua Kikuu na huduma nyingine za afya kwa ujumla kupitia jitihada zinazofanywa na serikali ikishirikiana na wadau mbalimbali hususani shirika la THPS Uhuru (Tanzania Health Promotion support) na AMREF Afya Shirikishi. Mwaka 2022 wagonjwa 1182 wa Kifua Kikuu waligundulika ikilinganishwa na wagonjwa 1092 mwaka 2021 ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.2. Wagonjwa (new and Relapse) 1028 kati ya wagonjwa 1092 wa Kifua Kikuu waliogundulika mwaka 2021 walitibiwa na kupona kwa asilimia 95.1 ikiwa ni zaidi ya lengo la Taifa la uponaji la asilimia 90.
3.3.2. HALI YA UGONJWA WA UKOMA MKOA
Mkoa umepiga hatua katika kupambana na Ugonjwa wa Ukoma kutoka wagonjwa 173 wa mwaka 2015 hadi wagonjwa 41 mwaka 2022.Hata hivyo Wilaya ya Nkasi bado haijafikia Kiwango cha kutokomeza Ugonjwa wa Ukoma ambapo ina kiwango cha maambukizi cha 1.2(prevalence rate).
Ili kuweza kutokomeza ukoma mikakati mbalimbali inaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya Ukoma, kufanya kampeni za kutokomeza Ukoma katika maeneo ambayo yana wagonjwa wengi (Hot spot area) hususani mwambao wa Ziwa Tanganyika wilaya ya Nkasi na kuhakikisha dawa mseto za Ukoma (Leprosy-MDT) zinapatikana muda wote, ili kuzuia na kutibu ulemavu utokanao na Ukoma.
3.3.3. Mafanikio katika kupambana na Kifua Kikuu na Ukoma
3.3.4. Changamoto katika kupambana na Kifua Kikuu na Ukoma
Pamoja na mafanikio mengi tuliyopata katika sekta ya afya, Mkoa bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza shughuli za kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma kama ifuatavyo;-.
3.4.0 Mapambano dhidi ya Malaria
Malaria ni moja kati ya magonjwa kumi yanayoongoza kwa kuwa kuwa na wagonjwa wengi wanaopata huduma za matibabu kwa wagonjwa ya nje (OPD) na wagonjwa wanaolazwa katika Mkoa
Kufuatia utafiti wa Malaria uliofanyika kwa wanafunzi wa shule za Msingi Mkoa wa Rukwa kati ya Julai hadi Agosti 2023 inaonyesha kuwa kiwango cha maambukizo ya Malaria kimepungua kutoka 17% kwa mwaka 2019 hadi 12% kwa mwaka 2023.
Halmashauri zote zimeonyesha kushuka kwa kiwango cha maambukizi ya Malaria isipokuwa Manispaa ya Sumbawanga ambapo imeongezeka kutoka 0.4% kwa mwaka 2019 hadi 1.7% kwa mwaka 2023.
Aidha takwimu za miezi sita ya Januari hadi Juni mwaka 2023 zinaonyesha kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria kimepungua kufikia wagonjwa 33,847 sawa na asilimia 8.6 ya wagonjwa wote waliotibiwa ukilinganisha na wagonjwa 48,191 sawa na asilimia 10 ya wagonjwa wote waliotibiwa kwa kipindi hicho cha mwaka 2022.
3.4.1. Jitihada za kupambana na Malaria
Kwa kuzingatia madhara yatokanayo na ugonjwa wa Malaria, Mkoa umekuwa ukichukua jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na;
Kugawa vyandarua kwa akina mama wajawazito na watoto wakati wa mahudhurio ya kliniki na makundi maalum (Wazee, Watoto wanaporuhusiwa baada ya kulazwa kutokana na ugonjwa wa Malaria na WAVIU). Aidha katika kipindi cha miezi sita ya Januari hadi Juni 2023 jumla ya vyandarua 34,912 sawa na asilimia 96 vilitolewa kwa akina mama wajawazito na vyandarua 37,666 sawa na asilimia 80 vilitolewa kwa watoto wanapohudhuria kliniki. Pia vyandarua 2791 vilitolewa kwenye makundi maalum.
Kusambaza mabango yenye ujumbe mbalimbali ambao unahamasisha jamii ‘kupima malaria, kwani si kila homa ni malaria, matumizi ya chandarua kujikinga na malaria, matumizi ya dawa kinga dhidi ya malaria kwa akina mama wajawazito na usafi wa mazingira.
Kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga dhidi ya malaria kupitia katika Radio zilizopo katika Mkoa ambazo ni pamoja na Voice FM na Ndingala.
Kuendesha vikao vya hamasa kwa viongozi mbalimbali mbali ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini, kimila na watu maarufu ili washiriki katika kuelimisha jamii.
Kuhamasisha jamii kuhusu usafi wa mazingira ili kuondoa mazalio na maficho ya mbu.
3.5. Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto.
Mkoa unaendelea na juhudi za kuboresha huduma za Afya ya uzazi na mtoto hususani katika kupunguza vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi. Hali halisi ya huduma na viashiria vya huduma hizi ni kama ifuatavyo;
3.6. Hali ya uwepo wa bidhaa za Afya na Uchunguzi.
Mkoa umeendelea kusimamia hali ya upatikanaji wa dawa, vifaatiba na vitendanishi katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya na kufikia mwezi Julai,2023, uwepo wa bidhaa za Afya katika vituo hivyo ni wastani wa asilimia 92% ambapo katika Manispaa Sumbawanga wana wastani wa 94% Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga 89 % Halmashauri ya Wilaya Nkasi 91% Halmashauri ya Wilaya Kalambo 93%
3.6.1. Matumizi ya fedha za bidhaa za Afya kupitia vyanzo mbalimbali Hadi Juni, 2023.
Jedwali Na.8.Matumiz ya Fedha
|
3.7. Mapato na Matumizi ya Fedha yatokanayo na Vyanzo mbalimbali katika Vituo vya kutolea huduma za Afya kwa Mwaka 2022/2023
Jedwali Na.9. Mapato na Matumizi ya Fedhakatika Halmashauri |
||||
Halmashauri
|
Bajeti
|
Mapato
|
Matumizi
|
Bakaa
|
HW Kalambo
|
2,037,850,156.69
|
1,714,491,254.12
|
1,543,919,374.36
|
170,571,879.76
|
HW Nkasi
|
3,227,719,635.18
|
3,046,879,434.84
|
2,690,757,328.01
|
356,122,106.83
|
HW Sumbawanga
|
2,171,003,453.79
|
1,061,098,701.54
|
707,833,099.58
|
353,265,601.96
|
Sumbawanga Manispaa
|
1,822,844,173.91
|
1,425,018,468.28
|
1,349,892,053.74
|
75,126,414.54
|
Jumla
|
9,259,417,419.57
|
7,247,487,858.78
|
6,292,401,855.69
|
955,086,003.09
|
3.7.1. Mapato na Matumizi ya Fedha yatokanayo na Makusanyo ya ndani (NHIF, DRF, UF, ICHF) katika Vituo vya kutolea huduma za Afya kwa Mwaka 2022/23 Jedwali Na.10.Mapato na Matumizi kwa fedha za ndani |
||||
Halmashauri
|
Bajeti
|
Mapato
|
Matumizi
|
Bakaa
|
HW Kalambo
|
220,582,212.05
|
728,225,517.35
|
679,224,251.89
|
49,001,265.46
|
HW Nkasi
|
550,974,183.32
|
622,262,093.80
|
516,377,526.19
|
105,884,567.61
|
HW Sumbawanga
|
240,760,335.91
|
253,239,759.06
|
109,586,428.02
|
143,653,331.04
|
Sumbawanga Manispaa
|
211,554,460.36
|
131,494,295.19
|
114,066,195.90
|
17,428,099.29
|
Jumla
|
1,223,871,191.64
|
1,735,221,665.40
|
1,419,254,402.00
|
315,967,263.40
|
3.7.2. Mapato na Matumizi ya Fedha za HSBF katika Vituo vya kutolea huduma za Afya kwa Mwaka 2022/23 Jedwali Na.11.Mapato na Matumiz kwa chanzo cha HSBF |
||||
Halmashauri
|
Bajeti
|
Mapato
|
Matumizi
|
Bakaa
|
HW Kalambo
|
980,147,999.59
|
571,357,833.54
|
531,760,478.07
|
39,597,355.47
|
HW Nkasi
|
468,954,010.15
|
610,832,756.54
|
506,081,654.56
|
104,751,101.98
|
HW Sumbawanga
|
585,300,315.88
|
668,198,929.46
|
470,727,908.56
|
197,471,020.90
|
Sumbawanga Manispaa
|
563,433,262.84
|
300,538,954.75
|
252,783,588.11
|
47,755,366.64
|
Jumla
|
2,597,835,588.46
|
2,150,928,474.29
|
1,761,353,629.30
|
389,574,844.99
|
Uhaba wa magari kwa ajili ya shughuli za usimamizi na usambazaji wa bidhaa za afya katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri.
Uhaba wa watumishi wenye ujuzi katika vituo vya kutolea huduma.
Uchelewaeshaji wa fedha kutoka serikali kuu katika ngazi ya Halmashauri na vituo vya kutolea huduma.
Uchache wa wadau wa maendeleo katika sekta ya Afya.
Baadhi ya vituo vya Afya vilivyokamilika kutokutoa huduma kwa sababu ya uhaba wa vifaa tiba.
Kushauri na kusimamia Halmashauri kutenga bajeti na kuomba vibali mbadala kwa watumishi wataalam kwa kada zenye uhitaji mkubwa.
Kuomba vyombo vya usarifi mfano magari na boti za kubebea wagonjwa.
Kuhakikisha vituo vinavyokamilika vinakuwa na watumishi na vifaa tiba vya utoaji wa huduma.
Kuwepo kwa mpango wa mafunzo kazini kwa ajili ya kuwaendeleza kitaaluma wataalam wa afya.
Kuendelea kusimamia mpango wa mkoa wa udhibiti wa magonjwa ya mlipuko.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa