• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

DED Kalambo na Timu yake Kuhojiwa na Kamati ya Ulinzi Mkoa kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya Waziri wa Uvuvi

imewekwa Tar: February 10th, 2020

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo pamoja na kamati aliyoundwa kutathmini miundombinu ya soko la samaki Kasanga kufika mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa kueleza sababu za kushindwa kutekeleza maagizo saba yaliyoachwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Mh. Luhaga Mpina juu ya uboreshwaji wa Soko hilo.

Waziri Mpina ambaye aliacha maagizo hayo alipofanya ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa tarehe 30.10.2019 na kujionea miundombinu chakavu iliyopo katika soko hilo pamoja na kusikiliza kilio cha wavuvi na wananchi wanaoishi karibu na soko hilo ambalo tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2013 na aliyekuwa makamu wa Rais Mh Dkt. Gharib Bilal halijawahi kutumika hadi leo.

Katika kusisitiza hilo Mh. Wangabo alisema kuwa miongoni mwa maagizo yaliyoachwa ni kuwa soko lianze kutumika kuanzia tarehe 31.12.2019 lakini halmashauri haina mpango huo, na kuongeza kuwa soko hilo ni chanzo cha mapato cha halmashauri kwani kukamilika kwake halmashauri itapata ushuru na kuongeza mapato katika halmashauri hiyo ambayo ipo hoi katika makusanyo na hivyo kuwataka watumie pesa kupata pesa.

“Wala msitegemee wizara ndio itafanya kila kitu hapa ili soko liweze kufanya kazi, lazima ninyi mtumie pesa ili mpate pesa, sasa kama hamtumii pesa kuuvuta umeme kutoka pale, ilikuwa ni changamoto kubwa mkasema hakuna transfoma tukamwambia meneja wa TANESCO leta transfoma akaleta ile pale mwaka jana, kutoa pale ule umeme kuja hapa imekuwa shughuli mnataka mwaka mwingine uishe, viongozi waendelee kutoka Dodoma, Dar es Salaam wanakuja hapa kwaajili ya mambo madogo madogo, haiwezekani, amkeni,” Alisisitiza.

Wakati akisoma taarifa ya mkoa juu ya utekelezaji wa maagizo hayo ya waziri Kaimu Katibu Tawala msaidizi seksheni ya Uchumi na Uzalishaji Respich Mayengo alisema kuwa Waziri mpina aliagiza kufanyika kwa maandalizi ya kuhakikisha kwamba soko la samaki linafanya kazi kuanzia tarehe 1.12020 na hivyo masuala yote yakamilike ndani ya miezi miwili kutoka 30.10.2019.

“Soko halijaanza kufanya kazi kwa kuwa mfumo wa umeme ndani ya soko haujakamilika licha ya kuwekewa transfoma, elimu na hamasa kwa wavuvi wa kata ya Kasanga na samazi haijatolewa na Katibu Tawala Mkoa alimwandikia DED Kalambo barua kuhusu kuanza kufanya kazi kwa soko hili na kutekeleza maelekezo ya waziri na kumpa ‘deadline’ ya terehe 20.1.2020 lakini hadi sasa barua hiyo haijajibiwa,” alisema.

Kwa upande wake katibu wa kamati hiyo Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sadick Senge alisema kuwa hivi karibuni wizara ilituma timu kufanya tathmini ya gharama (BOQ) kwaajili ya miundombinu ambayo wizara inaweza kuichukua na kuweza kuikarabati.

“Baadhi ya miundombinu hiyo ambayo wizara inaweza kuifanyia kazi ni Blast freezer, kuweka mashine na jengo la Soko lakini pia ilikuwa imefanya BOQ kwaajili ya mradi wa barafu na vilevile kuweka mtambo wa utakatishaji maji (water treatment plant) kwaajili ya kuzalisha barafu,” Alisema

Wakati alipopewa nafasi ya kuwasemea wavuvi wa Kata ya Kasanga Mwenyekiti wa Wavuvi hao Khalfan Saidi ameshauri kuwa umeme uwashwe ili mashine ya barafu ifanye kazi na barafu zikiwepo samakai watakuwepo, na kutahadharisha kuwa bila ya kuwepo kwa barafu hizo wavuvi hawawezi kuuza samaki wao kwenye soko hilo.

“Cha ajabu tangu wameweka transfoma pale kuunganisha tu umeme pale kwenye zile jenereta ili umeme uwake mwezi umeisha, kuunganisha tu pale mwezi umeisha kwahiyo imekuwa ni kila siku wakija tunazungumzia hili hili la kusema soko lifanye kazi, wavuvi wako tayari kuleta samaki hapa, sasa unamuamrishaje mvuvi kuleta samaki hapa hata barafu hakuna akileta samaki zake zisipouzikana hawezi kuhifadhi matokeo yake watu hukimbia na samaki zao vijiji, kwasababu vijijini kuna watu wenye friza wanatengeneza barafu,” Alisema.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa