Tuesday 21st, January 2025
@Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti leo (01.09.2021) ameongoza kika cha Kikao cha Kamati ya Kusimamia,Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Serikali Robo ya Nne 2020/21 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Sumbawanga ambapo ameagiza Wakurugenzi wote wa halmashauri kushirikiana kwa karibu na Wakaguzi wa Hesabu wa Ndani ili fedha zote zinaztolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi zitumike kikamilifu.
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka pia watendaji wa serikali kutumia sheria nakanuni za fedha katika kuhakikisha wananchi wananufaika na kodi zao kwenye kujiletea maendeleo.
Kikao hicho kimehusisha Katibu Tawala Mkoa Bw. Denis Bandisa, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakurugenzi wa Halmasahauri, Waweka Hazina wa Halmashauri na Wakaguzi wa Hesabu wa Ndani toka Halamashauri zote za Rukwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa