Wednesday 4th, December 2024
@
Mkoa wa Rukwa leo umezindua kampeni ya Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. kamapeni hii itakuwa kwa siku nne hadi tarehe 21 Mei mwaka huu ambapo lengo ni kuwafikia watoto 217,674 kote katika halmashauri za mkoa wa Rukwa. Uzinduzi umefanyika katika kituo cha afya Mazwi Manispaa ya Sumbawanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Joseph Mkirikiti.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa