Fomu ya Maombi ya Leseni za Biashara (TFN 211) kwa biashara ya kununua na kusafirisha Mifugo yanatakiwa kuambatishwa na nyaraka zifuatazo (Dully filled application Form (TFN 211) for Buying and Transportation of Livestock business license shall be accompanied by the following documents):-
A: Biashara ya Mifugo katika Mkoa
Mfanyabiashara anayefanya biashara ya kununua na kusafirisha mifugo yaani katika minada ya awali ndani ya mkoa anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:-
Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya/Manispaa husika kwa malipo ya shilingi 62,000/- na kupata Cheti Cha Usajili wa Wadau wa Sekta ya Nyama-Kutoka Bodi ya Nyama Tanzania.
Kitambulisho cha mwombaji wa leseni.
Uthibitisho wa Kuwa ana mahali pa Kufanyia biashara (Mfano. Mkataba wa pango wa Ofisi, Leseni ya Makazi au Hati).
Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA kinatolewa bila malipo
Kuwa na Tax clearance inayokokotolewa TRA.
Mfanyabiashara mwenye viambatisho husika atapewa Leseni ya kufanya biashara ya Mifugo ndani ya Mkoa husika. Leseni inatolewa na Ofisi ya Biashara ya Halmashauri kwa malipo ya kuanzia shilingi 80,000 na kuendelea kulingana na ada iliyopangwa na Halmashauri Husika.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa