Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha inaweka mikakati na mipango ya kulipa madeni ya watumishi na wazabuni yaliyobainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali katika taarifa ya ukaguzi ya kuishia Juni 30 Mwaka 2023.
Mheshimiwa Makongoro ameyasema hayo Juni 18, 2024 katika Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Sumbawanga kilichoketi kupitia na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amezitaka Halmashauri zote Mkoani Rukwa kuweka mipango na mikakati ya kulipa madeni yaliyobainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.
Pamoja na suala la madeni Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amezitaka Halmashauri kuhakikisha hazitumii fedha kabla ya kupelekwa benki na kutaka watumishi wote waliohusika kwa kutumia fedha kabla hazijapelekwa benki wachukuliwe hatua stahiki za kinidhamu na za kisheria
Aidha Mheshimiwa Makongoro amezitaka Halmashauri kusimamia vizuri miradi inayotekelezwa na kukamilika ili kutimiza azma ya Serikali na kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora.
Akihitimisha hotuba yake Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amezitaka Halmashauri kutumia mfumo wa NeST katika manunuzi ili kupunguza dosari zilizobainishwa na Mdhibiti na Mkgauzi wa Hesabu katika eneo la manunuzi
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa