Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imepongezwa kwa kupata hati safi kwa mwaka 2021/2022. Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 17 2023 aliposhiriki katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kupokea na kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha 2021/2022.
Pamoja na pongezi hizo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amelitaka Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kushirikiana na kuisimamia menejimenti ili kuhakikisha hoja zote zilizojitokea katika ukaguzi huo zinafanyiwa kazi kwa wakati ili kupunguza hoja zilizopo au kuzimaliza kabisa hoja hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imetakiwa kufanyia kazi hoja zilizojitokeza katika ukaguzi huo ikiwemo suala la ukusanyaji wa mapato na fedha kupelekwa benki kwa wakati , mapungufu katika usimamizi wa sheria na taratibu za manunuzi,kutokamilika kwa wakati kwa miradi ya maendeleo , na kutopeleka michango ya watumishi katika mfuko wa hifadhi ya jamii( PSSSF) .
Katika kikao hicho Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameagiza kuchukuliwa kwa hatua stahiki dhidi ya watumishi wote ambao wameisababishia Halmashauri hoja.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa