Maadhimisho ya siku ya hedhi salama yamefanyika leo tarehe 28 Mei, 2024 Mkoani Rukwa yakiongozwa na Mheshimiwa Nyakia Ally Chirukile, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mazoezi iliyopo Manispaa ya Sumbawanga na kuhudhuriwa na wanafunzi wa shule mbalimbali Mkoani Rukwa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo Mheshimiwa Chirukile amesema huduma bora za maji safi na salama zina mchango muhimu katika kuwahakikishia watoto wa kike hedhi salama.
Mheshimiwa Chirukile amewahimiza wazazi, wananchi na wadau wote kuhakikisha watoto wa kike wanapata maji safi na salama wakati wote kwa kusimamia vizuri rasilimali zilizopo na kusimamia kwa makini utoaji wa huduma.
Mheshimiwa Chirukile amesema kwa kufanya hivyo kauli mbiu ya mwaka 2024 isemayo kwa pamoja tuwezeshe mazingira rafiki na endelevu kwa hedhi salama itakuwa imetekelezwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa