Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mkoani Rukwa kuhakikisha miradi yote iliyipokea fedha kwa Mwaka 2022/2023 inakamilika ifikapo Oktoba 30,2023.
Ametoa maagizo hayo leo Oktoba 18,2023 alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Pia amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha kuwa miradi yote iliyoletewa fedha mwaka 2023/2024 inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa kulingana na maelekezo ya Serikali.
Amesema kuwa Mkoa wa Rukwa haupaswi kuwa na miradi iliyopita muda wa utekelezaji kwa kuwa hakuna changamoto ya fedha za utekelezaji wa miradi hiyo.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amekagua miradi sita ikiwemo mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga katika Kata ya Pito, ujenzi wa shule mbili mpya za Msingi katika Kata ya Msua na Momoka, ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Chanji, Ujenzi wa nyumba za walimu katika Shule ya Sekondari Aeish na ukamilishaji wa Zahanati ya Mponda.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa