Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere ametoa siku 14 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kukamilisha maabara katika Shule ya Sekondari Mazoezi iliyopo Kata ya Chanji.
Mheshimiwa Makongoro ametoa maelekezo hayo leo Juni 27, 2024 alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Sumbawanga.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amemtaka
Mkurugenzi kukamilisha ujenzi wa maabara ya masomo ya baolojia na kemia ifikapo tarehe 14 Julai 2024.
Agizo hilo linafuatia agizo kama hilo lililotolewa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tarehe 17 Mei 2024 alipofanya ziara ya ukaguzi shuleni hapo. Katika ziara hiyo ya Mei, Mheshimiwa Makongoro aliagiza mradi huo kukamilishwa ifikapo Juni 30 2024.
Shule mpya ya Sekondari ya Mazoezi inajengwa baada ya Manispaa kupokea kiasi cha Shilingi Milioni 530 kwa ajili ya ujenzi huo katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, huku lengo la ujenzi wa Shule hiyo likiwa ni kupunguza umbali kwa wanafunzi wa Kata ya Chanji na maeneo jirani.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa