Mkuu wa mkoa wa rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kwa kushirikiana na Wakala wa barabara mijini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanawaondoa wale wote waliokuwa wamejenga kwa kuifuata barabara na kusababisha ujenzi wa miundombinu kutekelezeka kwa ugumu.
“Zile barabara pale nendeni mkapitie ramani za mipango miji, kuna watu ninahakika walifuata barabara, ukiangalia kuna watu wapo kwenye mstari vizuri na wengine wameingia ingia kwenye barabara, fanyeni uhakiki yeyote yule ambae ameingia mtoeni tena hakuna gharama kwasababu ameifuata barabara,” Alisema
Aliyasema hayo alipofanya ziara ya mradi wa uboreshaji miji (ULGSP) unaodhaminiwa na benki ya dunia katika manispaa ya Sumbawanga na kubaini kuwa kuna baadhi ya nyumba zimezuia uchimbaji mzuri wa mitaro kwa kuingia ndani ya barabara na kuwafanya wajenzi hao kupindisha mitaro hiyo.
Awali akielezea vipengele vya mradi huo Meya wa manispaa ya Sumbawanga Justin Malisawa alisema kuwa Benki ya Dunia haina kipingele cha kulipa fidia na kuwa fidia hiyo ni mzigo wa halmashauri na hivyo kuwafanya wasibomoe nyumba za wakazi hao kwakuwa hawataweza kuwalipa fidia.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa