• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Wangabo atoa siku 5 wanafunzi kuripoti shule wazazi wasiotekeleza kushitakiwa

imewekwa Tar: January 28th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku tano kwa wazazi kuwaandikisha watoto waliofikisha umri wa kuanza shule pamoja na kuwafikisha shuleni wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ambao kwa mwaka 2020 wanafunzi 16,062 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika mkoa lakini hadi kufikia tarehe 24.1.2020 ni wanafunzi 11,149 pekee wameripoti ambao ni sawa na asilimia 69.41.

Aidha, katika kuhakikisha asilimia 100 inafikiwa amewaagiza watendaji wa Kata na vijiji mkoani humo kuwakamata na kuwashitaki kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009 wazazi wasiofanya hivyo na kuongeza kuwa sheria hiyo ya mtoto iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 inatamka wazi haki ya mtoto ikiwemo haki ya kupata elimu na kwa mzazi kutofanya hivyo ni kosa na adhabu yake ni kulipishwa faini au kufungwa jela ama vyote viwili kwa pamoja.

“Mimi natoa siku tano za wiki hii kwa wazazi wote ambao wana watoto hawajaenda shule mpaka sasa hivi iwe ni wa darasa la kwanza, wawe ni “form one” (kidato cha kwanza) baada ya siku hizi tano wakamatwe wafikishwe mahakamani hatutaki mchezo kwenye elimu, huyu mtoto ukimchezea chezea hivi huyu huyu ndio atatusumbua, kwasababu akitoroka shule anakimbia yamesmshinda ndio huyo anakwenda mitaani, unadhani watoto wa mitaani wanatoka wapi si wameshindwa shule huku, si wazaqzi wameshindwa kuwalea, wakamatwe wazazi wanashindwa kuwalea watoto wao wafikishwe mahakamani, watendaji wa vijiji watendaji wa kata kamateni wazazi hao” Alisisitiza.

Ameyasema hayo leo tarehe 27.1.2020 katika kikao kazi kilichohudhuriwa na watendaji wa vijiji na kata za Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga pamoja na watumishi wa halmashauri hiyo walioongozwa na makamu Mwenyekiti wa halmashauri pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga akianza ziara yake ya siku nne ya kukagua idadi ya wanafunzi walioripoti shule pamoja na mindombinu iliyopo. 

Mh. Wangabo amesema kuwa mkoa kufanya vibaya kwenye elimu kunachangiwa na kuchelewa kupeleka watoto shule na kuongeza kuwa endapo tathmini inafanyika kwa wale wanaofanya vibaya kwenye mitihani yao utagundua ni wale wanaochelewa kufika shule na kutahadharisha kuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapo katika kipindi cha mabadiliko kutoka kwenye ufundishwaji wa Kiswahili kwenda kwenye ufundishwaji wa kiingereza hivyo ni muhimu kwao kuwahi shuleni.

“Anatoka mazingira ya shule ya msingi anaingia ya sekondari , inapaswa mwanafunzi wa “form one” aanze mapema hata kabla ya shule kufunguliwa ili aaanze kuzoea zoea yale mazingira lakini hajafika mapema, shule imefunguliwa hayupo, mwezi mzima unapita hayupo shuleni , huyu hata “form two” unategemea atafaulu kweli?” Alihoji.

Halikadhalika, Mh. Wangabo amewataka watendaji hao kushirikiana na wenyeviti wa vijiji kuitisha mikutano ya vijiji na kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu kumuwahisha mtoto mapema shuleni huku wakiwabainishia faida na hasara za kutofanya hivyo na kuwaeleza juu ya umuhimu wa kusomesha watoto kwa maendeleo ya mkoa na nchi kwa ujumla.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni 4,394 huku walioripoti ni wanafunzi 2,973 ambao ni sawa na asilimia 67.7 huku wakihitaji madarasa 18 ambapo madarasa 15 tayari yamefikia usawa wa linta huku Mh Wangabo akitoa ahadi ya kuchangia mifuko ya saruji 150 ili kuwezesha kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa