Serikali kupitia Wizara ya Oisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kwaajili ya ujenzi wa viyuo vipya vya afya katika mkoa wa Rukwa ikiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu katika ngazi zote ambapo tayari mchakato wa ujenzi umeanza.
Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipokuwa akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichokaliwa tarehe 9.10.2018.
Mh. Wangabo amesema kuwa juhudi hizo zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano zitasaidia kuboresha afya za wananchi ikiwemo kupunguza masuala ya udumavu ambapo mkoa wa Rukwa una asilimia 56.3 na kupunga maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambayo yapo asilimia 4.4. kwa kupata elimu kupitia vituo hivyo.
“Serikali katika kuendelea kuipa kipaumbele Sekta ya Afya imeongeza idadi ya vituo vya afya vingine vitatu vijengwe ambavyo ni Kituo cha Afya Pito Katumba Tsh.400,000,000, Kituo cha Afya wapembe Tsh. 400,000,000 na Kituo cha Afya Kanyezi Tsh. 400,000,000 ambapo tayari mchakato wa ujezi umeanza.” Alisema.
Hapo awali serikali ilitoa shilingi bilioni 2.5 kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa vituo vya afya sita vya mkoa huo ikiwemo Kituo cha Afya Mazwi katika Manispaa ya Sumbawanga, Kituo cha Afya Nkomolo, Wilayani Nkasi, Vituo viwili vya afya vya Mwimbi na Legeza Mwendo, Wilayani Kalambo na kituo cha Afya Milepa katika halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa