Katika kuhakikisha wananfunzi wa shule ya sekondari Kala iliyopo kata ya Kala, Wilayani Nkasi wanapata uelewa wa kutosha na kuweza kuwashawishi wazazi wao kuanza kulima zao la alizeti shule hiyo imeanza kulima zao hilo ili kuona faida watakayoipata na hatimae kuwashawishi wananchi wanaozunguka shule hiyo kulima zao hilo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kala pia alimuomba mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kuweza kusaidia kuendelea kuwashawishi wananchi wa eneo hilo kuweza kulima zao hilo ambalo katika ekari moja ya shule iliyolimwa zao hilo inaonekana kufanya vizuri.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa katika kuitikia agizo lako uliowaita wadau na kuwashawishi kuhusu mazao ya biashara, sisi kama washawishi na watoa elimu tumeitikia kwa asilimia kubwa kwa kilimo cha Alizeti, tumejaribu kuanza ekari moja ya alizeti na linaenda vizuri, katika jitihafda hizi katika Kijiji cha King’ombe kata ya Kala ni sehemu ambayo alizeti inakuwa vizuri n ahata bila ya mbolea, tunakuomba uendelee kuwashawishi wananchi walime zao hili,” Alisema.
Nae, Mh. Wangabo aliipongeza shule hiyo kwa kuitikia wito wake na kuwa mfano bora kwa wananchi wa Kijiji cha King’ombe na hatimae kuweza kuwafundisha wananfunzi juu ya mtazamo wa zao hilo la kibiashara.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa