Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bw. Msalika Makungu leo Tarehe 30.09.2024 amepokea Timu ya Madaktari Bingwa 29 wa Kampeni ya afya ya Mama Samia ambao watatoa huduma mbalimbali za kibingwa katika Halmshauri nne za Mkoa wa Rukwa.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya madaktari hao Katibu Tawala wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kujitokeza wa wingi ili kupata huduma huku akitoa wito kwa madaktari kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi.
Awali akitoa taarifa ya ujio wa madaktari hao Bw. Ramadhan Masusu, mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amesema kuwa ujio wa wataalam hao ni ili kusaidia kutoa huduma za kibingwa kwa magonjwa ya watoto, magonjwa ya ndani, magonjwa ya akina mama na uzazi, kinywa na meno, usingizi na ganzi, upasuaji, mifupa na uuguzi.
Kwa upande wake Bw. Joachim Msungu mwakilishi wa Wizara ya Afya na kiongozi wa timu ya madaktari bingwa ameeleza kuwa lengo la Serikali ni kupunguza umbali wa upatikanaji wa huduma za rufaa kwa kusogeza huduma karibu na wagonjwa na kuwajengea uwezo wataalam wengine wa Afya ili waweze kutoa huduma hizo za kibingwa kwa wakati wote.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa