Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2023 Ndg. Abdalla Shaib Kaim amewata wananchi wa Mkoa wa Rukwa kutunza mazingira kwa kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji ili kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya mwenge wa Uhuru 2023 isemayo ”Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumba Haina Uchumi wa Taifa” .
Ndg Abdalla Shaib Kaim ametoa ujumbe huo alipokuwa akiongea na hadhara ya wananchi Wilayani Kalambo katika Kata ya Kasanga alipokuwa akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2023. Amewataka wananchi hao kuacha kuchoma moto hovyo, kutakata miti hovyo, kuepuka kutimia vifungashio vya plastiki na kuhifadhi vynazo vya maji ili kuweza kutekeleza kwa vitendo Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru na kuunga jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika utunzaji wa mazingira.
Mwenge wa Uhuru leo Agosti 30 2023 umezindua miradi 02, umeweka mawe ya msingi Miradi 02 na umekagua miradi 02 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.
Miradi iliyozindundiliwa ni miradi wa Maji Kata ya Kalaela wenye thamani ya Shilingi Milioni 436,uzinduzi wa Zahanati Kata ya Mbuza wenye thamani ya Shilingi Milioni 154 , Uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wenye Mahitaji Maalu shule ya Msingi Msanzi A yenye thamani ya shilingi Milioni 113, umeweka jiwe la msingi ujenzi wa Soko la Samaki katika kata ya Kasanga lenye Thamani ya Shilingi Milioni Bilioni 1.4 na kukagua mradi wa ujenzi wa Barabara ya Matai- Kisungamile kwa kiwango cha lami Km 1.5 na ukaguzi wa boti 02 za doria katika ziwa Tanganyika.
Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, RUWASA na TARURA wamepongezwa kwa kusimamia miradi vizuri ambayo inazingatia ubora pamoja na thamani ya fedha huku Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akisisitiza kuhakikisha maelekezo yote yaliyotolewa yanafanyiwa kazi.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa