Kukamilika kwa Zahanati ya Kijiji cha Katongolo Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa kunatajwa kuwapunguzia wananchi wa Kijiji hicho umbali wa zaidi ya kilomita 8 kufuata huduma za afya.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kirando , Dkt. Kenneth Timalasi ameyasema hayo mbele ya Mheshimiwa Makongoro Nyerere alipotembelea na kukagua ujenzi wa Zahanati hiyo tarehe 26 Juni 2024.
Serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 83 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo ili kutoa huduma za wagonjwa wa nje, mama na mtoto na huduma za maabara.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameishukuru Serikali kwa kuleta fedha za ukamilishaji wa Zahanati hiyo iliyochukua zaidi ya miaka kumi kukamilika.
Wananchi wa Katongolo wameishukuru Serikali kwa kukamilisha Zahanati hali ambayo imewapunguzia gharama za usafiri wa kufika katika kituo cha afya kilicho mbali na makazi yao na pia imepunguza vifo hasa vya kina mama wajawazito.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa