"Mkoa wa Rukwa upo pembezoni kabisa mwa nchi yetu upande wa kusini. Nataka niwaambie watanzania na kote duniani. Rukwa ni moja ya Mikoa yenye Fursa kiuchumi na maajabu ya kuvutia mno ya Kitalii kutokana na uwepo wa maliasili za kutosha ambazo hazijaendelezwa au kuwekezwa.
Rukwa ni mali mpya kwasababu rasilimali zake bado hazijaguswa hata kidogo na hasa katika vivutio vyake vya kitalii na uwekezaji wa Viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. hakuna sababu ya wawekezaji wa ndani ama wa nje kwenda kubanana kwenye maeneo ambayo tayari yanatumika kwa shughuli za kitalii.
kilichopo sasa na ni wito wangu kwa Wawekezaji wa ndani na wa nje wajitokeze na kuwahi kuwekeza katika fursa zenye maajabu ya vivutio vya kitalii na ukubwa wa Ardhi ya kuwekeza.
Na kwa kupitia tovuti hii unaweza kupata taarifa zitakazokuwezesha kufahamu fursa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wetu, kuanzia ngazi ya kijiji au mtaa hadi ngazi ya Mkoa, sasa hivi ulimwengu umerahisisha mambo mengi, ukiwa na simu yako tu yenye huduma ya 'internet' basi taarifa zote za mkoa unazipata humo. "
Mh. Joachim Wangabo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani
Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA
Simu: 025 280 2137
Simu: 0735019734
barua pepe: ras@rukwa.go.tz
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa