Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule ambaye pia alikuwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alikwenda kuzitembelea kaya 336 zilizoathiriwa na mvua na upepo mkali uliotokea usiku wa tarehe 8.12.2018 na kuahidi kutoa kilo 5 za unga wa sembe kwa kila kaya kama kianzio huku misaaada mingine ikiendelea kusubiriwa
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imeibuka mshindi wa kitaifa wa mbio za za Mwenge wa Uhuru uliowashwa mwezi April katika viwanja vya magogo Mkoani Geita na na kuzimwa mwezi oktoba siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl. Julius Nyerere katika Kiwanja Mkwakwani Mkoani Tanga na kukimbizwa katika Halmashauri 195 nchini.
Zao la kahawa ni miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo serikali ya awamu ya tano imeamua kwa dhati kutilia mkazo uzalishaji wake, kwa mkoa wa Rukwa zao hilo ndio zao ambalo limeonekana kustawi kwenye baadhi ya maeneo na kupelekea halmashauri za mkoa huu kutenga shilingi milioni 79 kwaajili ya kununua mbegu ili kuendeleza zao hilo.
Mkuu wa Mkoa wa rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema kuwa kama mkoa hatuna budi kutilia mkazo uanzishaji na uendelezaji wa zao hili ili wakulima wetu waweze kuwa na zao la biashara na kubainisha kuwa tayari maeneo kwaajili ya kilimo hicho yameshabainishwa ambapo makampuni, taasisi na wakulima wameonyesha nia ya kulima.
“Eneo la kiasi cha ekari 3,195.83 limebainishwa kwa ajili ya kulimwa zao la kahawa. Jumla ya wakulima 2,266 na taasisi 9 zitajihusisha katika uzalishaji wa kahawa. zikiwemo taasisi za Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania.”Alisema.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa