Uongozi wa Waislamu Mkoani Rukwa umepokea kwa furaha mchango wa Shilingi Milioni 5.7 uliotolewa na uongozi wa serikali ya Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika kikao cha maridhiano juu ya ujenzi wa msikiti uliosimama kwa muda. Fedha hizo zilizochangwa zilijumuisha ahadi, fedha taslimu pamoja na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa kwa umoja wa viongozi wa serikali kuonesha mshikamano uliopo kati ya serikali na wananchi bilaya kujali itikadi, dini wala rangi huku Mh. Wangabo akichangia milioni 1.5
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiwasilisha salamu za Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa waislamu wa Sumbawanga Mkoani Rukwa zikisisitiza kuendelea kwa ujenzi wa msikiti na kuendeleza mshikamano kujenga Rukwa moja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameitahadharisha bodi ya shule ya Sekondari Kantalamba kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuondoa daraja la sifuri katika shule hiyo kongwe nchini iliyoanzishwa mwaka 1964 na Kanisa Katoliki na hatimae kukabidhiwa rasmi serikali mwaka 1968.
Amesema kuwa shule hiyo haina hadhi ya kuwa na daraja la sifuri kutokana na kutoa viongozi mbalimbali walioiongoza nchi hii na kuwa serikali kwa makusudi imetoa shilingi Bilioni 1.1 ili kuboresha miundombinu ya shule hiyo hivyo haipendezi kusikika ikiendelea kutoa daraja la sifuri kuanzia kidato cha pili hadi cha sita.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa